• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama laeleza tena ufuatiliaji wake juu ya hali ya usalama huko Afrika Magharibi na Sahel

    (GMT+08:00) 2018-08-11 17:24:37

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeeleza tena ufuatiliaji wake juu ya "hali ya usalama yenye changamoto" katika Afrika Magharibi na Sahel, na kuyataka mashirika yake yaliyopo katika maeneo hayo kushirikiana ili kukabiliana nayo.

    Baraza hilo limetoa taarifa ya mwenyekiti likisema ugaidi, uharamia baharini, migogoro kati ya wafugaji na wakulima, pamoja na uhalifu unaovuka mipaka ya nchi vinatishia hali ya usalama kwenye maeneo hayo.

    Baraza hilo limepongeza juhudi zinazofanywa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya Afrika Magharibi na Sahel (UNOWAS) kwa kuunga mkono uchambuzi na utaratibu wa kutoa tahadhari mapema kuhusu suala hili katika kanda hiyo.

    Kuhusu uhalifu unaovuka mipaka, Baraza hilo limelaani tena biashara haramu ya binadamu, likisema inachangia kutokea kwa aina nyingine za uhalifu na inaweza kuongeza migogoro zaidi, na kusisitiza hitaji la kuhakikisha mpangilio na mapatano katika juhudi za Umoja wa Mataifa katika kushughulikia suala hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako