• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalam wamesema mabadiliko ya hali ya hewa yanatishia uzalishaji wa kahawa barani Afrika

    (GMT+08:00) 2018-08-11 17:41:30

    Mkurugenzi mtendaji wa Umoja wa Kahawa Bora wa Afrika Bw. Samuel Kamau amesema joto na muda mrefu wa ukame baada ya mvua kubwa kutokana na athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa vimeathiri vibaya upandaji wa kahawa barani Afrika na mwishoni vitaathiri uzalishaji.

    Bw. Kamau amesema hayo alipozungumza katika shughuli ya maandalizi ya awamu ya 17 ya Mkutano na Maonyesho ya Kahawa Bora ya Afrika. Ametoa wito kwa viongozi na watunga sera wa nchi za Afrika kuongeza juhudi na kuahidi kuchukua hatua za kimataifa na za kitaifa ili kupunguza athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa.

    Wakati huohuo, afisa mtendaji mkuu wa Bodi ya Kitaifa ya Maendeleo ya Uuzaji nje wa Mazao ya Kilimo ya Rwanda Bw. George William Kayonga amesema uzalishaji wa kahawa barani Afrika unatarajiwa kushuka kwa gunia milioni moja kutokana na hali ya hewa isiyotarajiwa, wadudu na majanga. Amesema nchi zinazozalisha kahawa za Afrika zinapaswa kushirikiana na wakulima wa kahawa kuibua mbinu mpya na zenye uvumbuzi ili kushughulikia changamoto kama vile mabadiliko ya hali ya hewa na masoko yanayobadilika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako