• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kufuzu Afcon 2019 U-17: Ethiopia, Rwanda, Sudan Kusini na Tanzania zapata ushindi mechi za kwanza

    (GMT+08:00) 2018-08-13 10:10:01

    Wikendi hii, timu za Tanzania, Rwanda, Sudan Kusini na Ethiopia zimepata ushindi katika mechi zake za kwanza za ngazi ya kanda ya Mashariki na Kati za kufuzu mashindano ya mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya Umri wa miaka 17 kwa mwaka 2019 zinazoendelea mjini Dar es Salaam.

    Tanzania ambao ni wenyeji waliifunga Burundi kwa magoli 2-1 katika mechi ya kundi A siku ya jumamosi, nao Rwanda siku hiyo hiyo walifanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-1 walipocheza dhidi ya Sudan.

    Katika mechi za kundi B zilizopigwa jana jumapili, Sudan Kusini ilipata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Djibouti, na Ethiopia ikapata ushindi wa goli 1-0 ilipocheza dhidi ya Uganda.

    Michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi za kundi A, ambapo Sudan itacheza dhidi ya Somalia, na Rwanda watacheza Burundi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako