• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wabunge wa Afrika watafuta mwafaka wa kuongeza ukuaji wa sekta ya ICT

    (GMT+08:00) 2018-08-13 19:51:19

    Wabunge wa Afrika wamekubaliana kuwa na msimamo wa pamoja katika kuchochea ukuaji wa sekta ya teknolojia ya upashanaji habari (ICT) na kuiongeza kwenye ajenda ya mageuzi ya bara hilo.

    Wabunge hao na wataalam walikutana mjini Nairobi, Kenya katika mkutano wa maandalizi kabla ya Mkutano wa Shirika la Kimataifa la Mawasiliano ya Simu (ITU) utakaofanyika Dubai mwezi Oktoba. Wamesema mwafaka unatakiwa ili kuharakisha mageuzi ya nne ya kiviwanda barani Afrika ambayo msingi wake ni teknolojia na uvumbuzi.

    Nchi za Afrika zimeungana katika kutafuta ukuaji wa kasi wa sekta ya ICT ambayo itasaidia kukabiliana na changamoto za kijamii na kiuchumi barani humo kama vile umaskini, magonjwa, na uharibifu wa mazingira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako