• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda ilifungua mashtaka zaidi ya 200 dhidi ya watuhumiwa wa mauaji ya kimbari mwaka jana

    (GMT+08:00) 2018-08-14 09:08:06

    Idara ya mashtaka ya Rwanda mwaka jana ilifungua mashtaka 218 dhidi ya watuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Mwendesha mashtaka mkuu Bw. Jean Bosco Mutangana amesema watuhumiwa hao wanaishi katika nchi 14 za Ulaya na Afrika, na zaidi ya mashtaka elfu moja yalifunguliwa dhidi yao katika miaka kumi iliyopita.

    Bw. Mutangana amezilaani baadhi ya nchi kutotaka kuwakabidhi watuhumiwa hao kwa Rwanda, na kutoa wito kwa nchi hizo kufanya juhudi kuhakikisha watuhumiwa hao wanarudishwa Rwanda au kusikilizwa kesi zao katika nchi hizo ili wasikwepe adhabu wanazostahili kisheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako