• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki kuu ya Uganda yakadiria uchumi kukua kwa asilimia 6.3

    (GMT+08:00) 2018-08-14 09:16:49

    Benki kuu ya Uganda imesema uchumi wa Uganda unatarajiwa kukua kwa asilimia 3.6 katika kipindi cha kati. Gavana wa Benki hiyo Bw. Emmanuel Mutebile amewaambia wana habari kuwa ongezeko la uchumi linazidi kuimarika, huku pato la taifa kwa mwaka huu wa fedha likiendelea kuongezeka kwa asilimia 5.5, ilikinganishwa na asilimia 3.9 za mwaka wa fedha uliopita.

    Ongezeko hilo litatokana na uwekezaji kwenye ujenzi wa miundombinu, kuboresha uzalishaji wa kilimo, kufufuka kwa uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje, na kuimarika kwa sekta ya mikopo binafsi, ikiwa ni sehemu ya matokeo ya kulegeza sera ya fedha.

    Hata hivyo Bw. Mutebile amesema kuna changamoto kuhusiana na uwekezaji kwenye miradi ya umma, na mfumuko wa bei unaoweza kufikia asilimia 6 hadi 7.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako