Mechi za Simba na Yanga hazitachezwa katika uwanja wa taifa kutokana na wamiliki wa uwanja huo ambao ni serikali kuwa na matumizi nao.
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi Boniface Wambura ameeleza kuwa Wizara ya michezo imeiandikia barua bodi ya Ligi, kuwa hautaruhusiwa kutumika kuanzia August 22 hadi September 1 2018 kwa mechi za Ligi, ndiyo sababu kubwa ya kulazimika kuhamisha baadhi ya mechi ambazo sasa zitachezwa katika uwanja wa uhuru.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |