• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni za China zapanua uagizaji wa bidhaa kutoka nchi mbalimbali duniani ili kukabiliana na mgogoro wa kibiashara na Marekani

  (GMT+08:00) 2018-08-14 18:30:02

  Tangu mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani uliopotokea, kampuni nyingi za chakula za China ikiwemo Kampuni ya COFCO zimepanua eneo la kuagiza soya kutoka nchi za nje ili kukabiliana na changamoto zinazoletwa kutokana na kupunguzwa kwa uagizaji wa soya kutoka Marekani.

  China ikiwa nchi kubwa zaidi inayoagiza soya kutoka nchi mbalimbali duniani, thamani yake ya kuagiza soya kutoka nchi za nje kwa mwaka inachukua takriban asilimia 60 ya thamani ya jumla ya dunia, na uagizaji wa China wa soya kutoka Marekani unachukua asilimia 60 ya uuzaji wa soya wa Marekani katika nchi za nje. Tangu Marekani ilipochochea mgogoro wa kibiashara mwaka huu, ikiwa moja kati ya hatua za kuijibu Marekani, China imeongeza ushuru kwa asilimia 25 kwa soya za Marekani, na gharama za uagizaji wa soya kutoka Marekani zimeongezeka kwa RMB yuan 700 hadi 800 kila tani, kiasi ambacho kinazidi kwa yuan 300 kutoka soya zinazoagizwa kutoka Brazil, na soya za Marekani zimepoteza sifa yake ya ushindani katika soko la China.

  Meneja mkuu wa kundi la COFCO ambayo ni kampuni kubwa ya kwanza ya mafuta na chakula ya China, na ya tano ya duniani, Bw. Yu Xubo anasema:

  "Takwimu zinazotolewa katika nusu ya kwanza ya mwaka huu zimeonesha kwua, uagizaji wa soya wa China kutoka Marekani umepungua kwa asilimia 16, huku uagizaji wa soya kutoka Latin Amerika umeongezeka kwa asilimia 15 haswa nchini Brazil."

  Wachambuzi wanaona kuwa, endapo mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani ukiendelea, uagizaji wa soya wa China kutoka nchi za Latin Amerika na zile zinazojiunga na pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" utaweza kuzidi kuongezeka. Nchi mbalimbali zilizoko Latin Amerika zikiwemo Brazil, Argentina na Uruguay zina maeneo makubwa ya ardhi zenye rutuba nyingi, ambazo zitakuwa nguvu muhimu ya ongezeko la uzalishaji wa soya katika siku za baadaye. Mbali na hayo, nchi mbalimbali zinazojiunga na pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" zikiwemo Russia, Ukraine na Kazakhstan vilevile zina maliasili nyingi ya ardhi na uwezo mkubwa wa uzalishaji. Katika miaka mitatu iliyopita, uuzaji wa soya wa Russia katika nchi za nje utaongezeka kwa zaidi ya asilimia 150.Bw. Yu Xubo anasema:

  "Kutokana na mwelekeo wa muda mrefu ujao, eneo kubwa la mashamba katika nchi za Latin Amerika na Bahari Nyeusi lina sifa kubwa sana ambayo yataweza kuchangia zaidi katika mfumo wa utoaji wa soya. Kuagiza soya kutoka nchi tofauti kutatoa uthibitisho imara kwa utoaji wa mazao ya kilimo na chakula kwa China, na pia kutaleta fursa muhimu kwa nchi nyingine duniani."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako