• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: TPA inatarajia kuhudumia tani milioni 14 za shehena

    (GMT+08:00) 2018-08-14 20:00:38

    Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (,TPA inatarajia kuhudumia tani 14374,400) yakiwemo makontena (TEUs) 208,000 katika vitengo vinavyoendeshwa na mamlaka hiyo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019.

    Kitengo cha Kontena katika Bandari ya Dar es Salaam (TICTS) pia kinatarajia kuhudumia makontena (TEUs) 489,300 katika mwaka huo wa fedha.

    Mkurugenzi Mkuu wa (TPA), Deusdedit Kakoko amesema hayo Dar es Salaam wakati akielezea mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 ya mamlaka hiyo.

    Pia alisema wanatarajia kuhudumia meli 2,736 zenye ukubwa wa (GRT) milioni 35.880 na kati ya hizo meli 1,307 ni za Kimataifa (Deep Sea), meli 786 ni za mwambao na meli 670 zitahudumiwa katika bandari za Maziwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako