• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani yaendelea kuinua kigezo cha uwekezaji wa kigeni nchini humo

  (GMT+08:00) 2018-08-15 19:01:42

  Hivi karibuni, Marekani imetoa muswada wa sheria wa mageuzi ya ukaguzi wa usalama wa taifa dhidi ya uwekezaji wa kigeni. Hii ni mara ya kwanza kwa Marekani kurekebisha na kuimarisha uwezo wa kamati ya uwekezaji wa kigeni katika miaka karibu kumi iliyopita. Kamati hii itafanya ukaguzi mkali zaidi kwa uwekezaji wa kigeni unaotaka kuingia nchini Marekani.

  Lakini ukweli ni kwamba, historia ya Marekani kufanya ukaguzi wa usalama dhidi ya uwekezaji wa kigeni ni ndefu sana. Kamati ya uwekezaji wa kigeni ya Marekani iliyozinduliwa mwaka 1975, ina mamlaka ya kuamua kama kampuni inawekeza au kununua kampuni nyingine. Kufuatia hatua ya ulinzi wa biashara inayochukuliwa na serikali ya Marekani ya awamu hii, mswada wa sheria wa mageuzi ya ukaguzi wa usalama wa taifa dhidi ya uwekezaji wa kigeni umetungwa.

  Katika miaka kadhaa iliyopita, wakati Marekani ilipozuia uwekezaji wa kigeni, ilikuwa inatumia kisingizio cha msingi cha kulinda usalama wa taifa. Mpaka sasa, Marekani daima inashika hadhi ya utawala kwenye sekta za siasa, uchumi, mambo ya kijeshi na teknolojia, na bado hakuna nchi yoyote inayoweza kutishia usalama wa Marekani. Hivyo, nyuma ya kisingizio hicho, ni kuwa Marekani ina wasiwasi kuhusu viwanda vyake na uvumbuzi wa teknolojia utashindwa na nchi nyingine. Marekani haitilii maanani mawimbi ya maendeleo ya utandawazi, na kuweka kizuizi ili kuzuia washindani wengine kupata teknolojia mpya na kutikisa hadhi yake.

  Wachambuzi wanaona kuwa, kizuizi kilichowekwa na Marekani dhidi ya mitaji ya kigeni kitaharibu fursa ya maendeleo ya kampuni za nchi hiyo na kupunguza nafasi za ajira ndani ya muda mfupi, pia kitaleta athari mbaya zaidi kwa maendeleo ya viwanda na ubunifu wa teknolojia. Kwa sababu katika zama ya mafungamano ya kiuchumi duniani, mashirika ya kimataifa yana nia na mahitaji ya kufanya ushirikiano katika kuzidisha uwekezaji na mawasiliano ya teknolojia, ambayo haitakiwi kutekwa nyara na faida binafsi ya wanasiasa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako