Ongezeko hili la bei linakuja kama kionjo tu kwa bidhaa zote za petroli kwani kuanzia mwezi ujao Hazina ya Taifa itaanza kutoza ushuru wa thamani kwa petrol,hivyo bei hiyo inatarajiwa kuongezeka zaidi.
Kulingana na muongozo wa bei unaotolewa na ERC kila mwezi,uliotolewa tarehe 14 Agosti,petrol sasa itauzwa Sh113.73 jijini Nairobi,kutoka Sh112.2 mwezi uliopita.
Watumizi wa mafuta ya dizeli watapata nafuu kiasi,huku lita moja ya bidhaa hiyo ikipungua kwa senti 51 hadi Sh102.74.
Nyumba zinazotegemea mafuta ya taa pia zitapata afueni baada ya tume ya ERC kupunguza bei ya mafuta hayo kwa senti 78 hadi Sh84.95 kwa lita.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |