• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" wasaidia ushirikiano kati ya China na Afrika katika kupunguza umaskini

    (GMT+08:00) 2018-08-16 09:07:30

    Mkutano wa mwaka 2018 kuhusu upunguzaji umaskini na maendeleo chini ya baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC umefunguliwa Jumanne mjini Beijing. Wajumbe wanaohudhuria mkutano huo wamejadiliana kuhusu wazo jipya na njia mpya za kushirikisha pande nyingi za serikali, viwanda, duru za kisomi, mashirika ya kimataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na kuhimiza ushirikiano kati ya China na Afrika katika juhudi za kupunguza umaskini.

    Mkurugenzi wa ofisi ya kupambana na umaskini ya baraza la serikali ya China Bw. Liu Yongfu, amesema kwenye mkutano huo kuwa China na Afrika zina mchakato unaofanana wa kujiendeleza, na kuondoa umaskini na kutimiza maendeleo endelevu ni lengo na majukumu ya pamoja ya watu wa China na Afrika. Pande hizo mbili zinahitaji kuimarisha mawasiliano, kujenga mfumo wa ushirikiano wa kupunguza umaskini chini ya mfumo wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na kuendelea kuhimiza ushirikiano katika kupunguza umaskini.

    "katika miaka mitano iliyopita, pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" limetimizwa hatua kwa hatua, nchi na mashirika ya kimataifa zaidi 100 zikiwemo nchi za Afrika zimeshiriki kwenye ujenzi huo, miradi mingi ya ushirikiano imetekelezwa, mtandao wa mawasiliano ya miundo mbinu umekuwa na muundo wa mwanzo, uratibu wa kisera wa nchi mbalimbali umeimarika, na watu wa nchi zilizoko kwenye Ukanda mmoja Njia moja wamenufaika zaidi. Thamani ya jumla ya biashara kati ya China na nchi hizo imefikia zaidi ya dola za kimarekani trilioni 5, uwekezaji umezidi dola za kimarekani bilioni 70, na kuongeza nafasi za ajira zaidi ya laki 2. Hayo yote yamethibitisha kuwa, kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja na Njia Moja" ni njia ya kunufaishana ya kusukuma mbele maendeleo ya kiuchumi na kijamii, kuhimiza juhudi za kuondoa umaskini na kutimiza maendeleo ya pamoja."

    Mwaka 2018, China zilisaini hali ya maelewano kuhusu kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na Senegal na Rwanda, na kuafikiana na Mauritius kuhusu kusaini makubaliano ya kujenga "Ukanda Mmoja na Njia Moja". Waziri wa ushirikiano wa jamii na ukuaji wa uchumi wa Mauritius Bw. Marie Roland Alain, amesema ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" umetoa fursa mpya kwa ajili ya ushirikiano wa kuondoa umaskini kati ya China na Afrika.

    "China imepata mafanikio makubwa katika kuondoa umaskini. Katika miaka ya hivi karibuni, China imewasaidia watu milioni 10 kuondokana na umaskini kila mwaka, na inapanga kutimiza lengo la kutokuwa na watu maskini kabisa ifikapo mwaka 2020. China ina uzoefu mkubwa wa kuondoa umaskini ili kuzisaidia nchi za Afrika kujiendeleza, na nchi za Afrika zinahitaji kuunganishwa kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja". China siyo tu inatoa teknolojia, fedha na vifaa, pia inatoa msaada wa watu. Vilevile China inatusaidia kuondoa umaskini na kutuletea teknolojia na ustadi hizo siyo kwa mtizamo wa washindani, bali ni wenzi wa ushirikiano."

    Utafiti wa chuo kikuu cha kilimo cha China umeonyesha kuwa, pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" limehimiza kupunguza umaskini kupitia kuhamisha uwezo wa uzalishaji viwandani, kuwekeza kwenye sekta za kilimo na miundo mbinu. Kwenye mkutano huo katibu mkuu mtendaji wa mkoa wa Morogoro Tanzania Bw. Clifford Tandari amefahamisha hali ya utendaji wa kituo cha kwanza cha kijijini cha mafunzo ya kupunguza umaskini barani Afrika kilichojengwa na kituo cha kupambana na umaskini cha China. Amesema kituo hicho kimetoa mafunzo ya teknolojia na usimamizi kwa wenyeji, kuinua uzalishaji wa kilimo na kupunguza idadi ya watu maskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako