Ronaldo alifunga bao hilo la kushangaza la 'bicycle-kick' na kuwasaidia Real Madrid kuwalaza Juventus 3-0 katika mechi ya mkondo wa kwanza ya robofainali katika ligi ya klabu bingwa Ulaya.
Alikuwa pia amefunga bao la kwanza kwenye mechi hiyo na kwa mabao yote mawili aliandika historia.
Kwa jumla, kuna mabao 11 ambayo yanashindania tuzo hiyo, ambapo kuna pia bao alilolifunga Mwingereza Lucy Bronze wa timu ya kinadada ya Lyon ya Ufaransa dhidi ya kina dada wa Manchester City.
Vilevile, Bao la kiungo wa Tottenham Christian Eriksen wakati wa mechi ya muondoano wa kufuzu kwa kombe la Dunia baada ya hatua ya makundi dhidi ya Jamhuri ya Ireland pia limeorodheshwa kushindania tuzo hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |