• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutumia fursa ya maendeleo ya nchi hiyo

  (GMT+08:00) 2018-08-16 19:35:55

  Takwimu za uchumi zilizotolewa mwezi wa Julai na serikali ya China zinaonesha kuwa, thamani ya jumla ya mauzo na uagizaji bidhaa kutoka nje imefikia dola bilioni 377.4 za kimarekani, ambayo iliongezeka kwa asilimia 12.5 kwa kulinganishwa na ya mwezi wa Juni. Glorie Ngahyoma na maelezo zaidi:

  Thamani ya mauzo ya bidhaa imefikia dola bilioni 201.5 za kimarekani, huku thamani ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje ikifikia dola bilioni 175.9 za kimarekani. Kwa kulinganisha thamani ya mauzo na ya uagizaji, faida ya biashara imefikia dola bilioni 25.6 za kimarekani, ambayo imepungua kwa dola bilioni 12.1 za kimarekani ikilinganishwa na mwezi Juni.

  Takwimu hizo zinaonesha kuwa, sera ya kufungua mlango zaidi inayofuatwa na China imeleta faida nyingi zaidi kwa nje. Kama rais Xi Jinping wa China alivyosema kwenye mkutano wa mwaka 2017 wa Baraza la Uchumi la Dunia, maendeleo ya China ni fursa ya dunia, na China inakaribisha nchi mbalimbali kunufaika kwa pamoja na China .

  Katika nusu ya pili ya mwaka huu, China italeta faida mbili kubwa kwa dunia. Ya kwanza, China itazindua mawasiliano kati ya soko la hisa la Shanghai na la London ili kuzidi kufungua soko la fedha. Ya pili ni kuwa China itafanya Maonesho ya kwanza ya Mauzo ya Bidhaa na Uagizaji wa Bidhaa kutoka nje ya China mjini Shanghai, ili kutoa soko na jukwaa kubwa zaidi la biashara kwa wenzi wa biashara wa kimataifa na kuleta mahitaji ya soko.

  China sio tu ina soko kubwa lenye watu karibu bilioni 1.4, bali pia ina nia thabiti ya kuunga mkono biashara huria na urahisishaji wa uwekezaji. Wawekezaji na wafanya biashara hawawezi kupata soko kubwa zaidi kuliko China, hivyo wanachotakiwa kufanya ni kushika fursa hiyo na kupanda treni ya mwendo wa kasi ya maendeleo ya China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako