• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • ULAYA: Ufaransa yakaa kileleni viwango vya soka duniani

  (GMT+08:00) 2018-08-17 09:53:21

  Ufaransa imekamata nafasi ya kwanza katika viwango vya ubora wa soka duniani mwaka huu ikiwa imepanda kwa nafasi sita ikifuatiwa na Ubelgiji ambayo imepanda kwa nafasi moja. Brazil imekamata nafasi ya tatu ikishuka kwa nafasi moja huku Croatia ikiwa imepanda kwa nafasi 16 hadi nafasi ya nne.

  Kwa upande wa bara la Afrika, Tunisia inaongoza ikiwa nafasi ya 24, sawa na Senegal ambayo imepanda kwa nafasi tatu, zikifuatiwa na DRC iliyo nafasi ya 37, Ghana nafasi ya 45, Morocco nafasi ya 46, Cameroon nafasi ya 47 na Nigeria ikiwa nafasi ya 49 baada ya kushuka kwa nafasi moja.

  Na Afrika Mashariki inaongozwa na Uganda ambayo imebaki nafasi ya 82 ikifuatiwa na Kenya nafasi ya 112, Rwanda nafasi ya 136, Tanzania nafasi ya 140, Burundi nafasi ya 148 na Sudan Kusini ikiwa nafasi ya 156.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako