• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakazi watishia mradi wa unyunyizaji mashamba Lower Nzoia

    (GMT+08:00) 2018-08-17 20:16:15

    Wakazi wa eneobunge la Budalang'i sasa wanasema watasambaratisha mradi wa unyunyizaji mashamba wa Lower Nzoia iwapo serikali itaendelea kulifumbia macho swala la kuwafidia. Wakazi hao wanahofia kupoteza vipande vyao vya ardhi iwapo mradi huo utakaogharimu serikali Sh10 billioni utaanzishwa kabla ya wao kulipwa fidia. Wakazi hao walisema kuwa hawatakubali mkandarasi kuanza kazi kabla ya kupata fidia kutoka kwa tume ya ardhi nchini (NLC). Malalmishi ya wakazi yanajiri majuma machache tuu baada ya waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa kuitaka NLC kuharakisha shughuli ya kuwafidia ili kutoa nafasi kwa mradi kuanza baada ya kucheleweshwa kwa zaidi ya miezi minne.

    Machi 2018 naibu mkurugenzi wa bodi ya unyunyizaji mashamba (NIB) Daniel Atula aliwahakikishia wakazi kuwa watafidiwa kwa mujibu wa sheria.

    Katika awamu ya kwanza ya mradi huo, takriban 34 kilomita za kingo zinatarajiwa kukarabatiwa.

    Awamu hii inalenga kuwafaidi zaidi ya wakazi 78,000 katika eneobunge la Budalangi na maeneo jirani.

    Mradi wa unyunyizaji mashamba wa Sisenye utaanzishwa katika awamu ya pili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako