• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa asema mkutano ujao wa kilele wa China na Afrika utapata mafanikio

    (GMT+08:00) 2018-08-18 16:15:27

    Kamishna wa masuala ya kijamii wa Umoja wa Afrika Amira Elfadil ameeleza matumaini yake kuwa, mkutano ujao wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utapata mafanikio.

    Akizungumza wakati wa kupokea hati za utambulisho wa balozi wa China kwenye Umoja huo Bw. Liu Yuxi, Bw. Elfadil amesema Tume ya Umoja wa Afrika itachukua nafasi kubwa kwa kushiriki kwenye mkutano huo wa kilele utakaofanyika mapema mwezi ujao hapa Beijing. Amesema mkutano wa kilele wa FOCAC umekuwa mkutano wa kawaida kati ya Afrika na China na kuna mpango mkubwa utakaokuja kutokana na ushirikiano huo ndani ya mkutano wa FOCAC.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat pamoja na wajumbe wengine wa ngazi ya juu wa Umoja huo watahudhuria mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako