• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yawarudisha kwa hiari wakimbilizi zaidi ya elfu 80 wa Somalia kutoka Kenya

    (GMT+08:00) 2018-08-18 16:15:50

    Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema kuwa limewarudisha kwa hiari wakimbizi 81,451 wa Somalia kutoka Kenya mpaka kufikia Julai 31 tangu zoezi hilo lilipoanza Disemba mwaka 2014.

    Katika ripoti yake ya kila mwezi, Shirika hilo limesema wakimbizi 6,085 walirejeshwa Somalia kwa mwaka huu, na kuongeza kuwa wakimbizi 191 wa Burundi pia walisaidiwa kurejea nchini mwao mwaka huu.

    Kenya, ambayo ilianzisha majadiliao yaliyohitimishwa kwa kuanzisha serikali ya mpito ya Somalia, imesema hali ya wakimbizi inaendelea kutishia usalama wa Kenya na kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako