• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China itaendelea kuimarisha ushirikiano kati yake na Iran

    (GMT+08:00) 2018-08-18 17:00:29

    Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje Bw. Wang Yi amesema China inathamini uhusiano kati yake na Iran na inataka kuendelea kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana kati ya pande hizo mbili kwa mujibu wa hali ya maendeleo.

    Bw. Wang Yi alisema hayo jana alipozungumza na waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw. Mohammad Javad Zarif kwa njia ya simu. Amesema makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 ni mafanikio muhimu ya utaratibu wa pande nyingi kwa kulingana na maslahi ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa. Ameongeza kuwa China inapinga nchi moja kuweka vikwazo ama kutumia madaraka ya kisheria dhidi ya nchi nyingine kwa kutumia sheria yake yenyewe.

    Kwa upande wake, Bw. Zarif ameiarifu China kuhusu maendeleo mapya ya suala la nyuklia la Iran na kusisitiza kuwa Iran inathamini nafasi ya kiujenzi inayofanywa na China katika kudumisha makubaliano ya nyuklia ya Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako