• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatuma madaktari zaidi ya 2,000 wa matibabu ya jadi ya kichina barani Afrika

    (GMT+08:00) 2018-08-19 18:21:57

    Mkurugenzi wa idara ya taifa ya usimamizi wa tiba na dawa za jadi za China Bw. Yu Wenming, amesema serikali ya China imetuma madaktari zaidi ya 2,000 wa matibabu ya jadi ya kichina barani Afrika, na kutoa huduma za tiba na dawa za jadi za kichina kwa waafrika kwa njia ya matibabu na utafiti wa kisayansi.

    Bw. Yu Wenming amesema hayo jana katika kongamano la ushirikiano wa tiba na dawa za jadi za kichina kati ya China na Afrika. Amesema serikali ya China imesaini makubaliano na Ghana, Tanzania, visiwa vya Comoro, Malawi na Ethiopia kuhusu tiba hiyo.

    Tiba na dawa za jadi za kichina zimejiunga na huduma za afya za waafrika, na kutoa mchango mkubwa kwa nchi za Afrika katika kukinga na kutibu magonjwa makubwa ya kuambukizwa, magonjwa ya kawaida na huduma za afya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako