• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UNCTAD asema mfumo wa FOCAC unahimiza biashara kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-08-20 09:49:52

    Katibu mkuu wa Mkutano wa biashara na maendeleo wa Umoja wa Mataifa UNCATD Bw. Mukhisa Kituyi amesema chini ya msukumo wa mfumo wa baraza la ushirikiano wa China na Afrika FOCAC, biashara kati ya China na Afrika inaendelea kuboreshwa.

    Bw Kituyi amesema katika miaka ya karibuni msingi wa biashara kati ya China na Afrika umezidi kuimarishwa chini ya mfumo wa FOCAC, na biashara kati ya pande mbili imeingia kwenye kipindi kipya. Bidhaa za Afrika zinazouzwa China si malighafi zilizoshughulikiwa kwa hatua ya mwanzo tu, ikiwa ni pamoja na chuma cha pua, mafuta na mazao ya kilimo, bali pia bidhaa zilizotengenezwa zimeanza kuingia nchini China. Amesema kuanzishwa kwa eneo la biashara huria la Shanghai kumeipatia Afrika fursa ya kuuza bidhaa nchini China, pia kumepunguza urari mbaya wa Afrika katika biashara kati yake na China.

    Bw. Kituyi ameongeza kuwa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" lililotolewa na rais Xi Jinping wa China limehimiza maendeleo ya biashara kati ya China na Afrika, na pia limesaidia nchi za Afrika zipate maendeleo kwenye sekta ya ujenzi wa viwanda. Mashirika ya China yanazisaidia nchi za Afrika kujenga viwanda na kuongeza nguvu ya ushindani ya bidhaa zao kwenye soko la dunia nzima. Mambo hayo yote yanaonyesha kwamba China na Afrika ni wenzi wa ushirikiano wa biashara wa kunufaishana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako