• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Balozi wa Zimbabwe nchini China aeleza ushirikiano kati ya China na Zimbabwe

  (GMT+08:00) 2018-08-21 08:57:04

  "Katika makumi ya miaka iliyopita, China na Afrika zimeshirikiana na kushikamana kwa dhati. Zinadumisha hali ya kuwa jumuiya yenye hatma na maslahi ya pamoja." Hayo yamesemwa na rais Xi Jinping wa China wakati alipotembelea Afrika mwezi Juni, mwaka huu. Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika. FOCAC utakaofanyika hivi karibuni, unafuatiliwa sana duniani. Kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo, waandishi wa habari wa CRI wamefanya mahojiano na mabalozi wa Tanzania, Zimbabwe, Rwanda, Uganda, Burundi na Afrika Kusini nchini China, kuhusu mafanikio na maendeleo yaliyopatikana chini ya mfumo wa FOCAC, kuhimiza ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja ili kupata maslahi ya pamoja ya China na Afrika. Hivi karibuni tumemhoji balozi wa Zimbabwe nchini China Bw. Paul Chikawa akieleza ushirikiano kati ya China na Zimbabwe.

  Mwanahabari: Uhusiano kati ya China na Zimbabwe imekuwa mzuri tangu ianzishwe. Unaonaje uhusiano huu?

  Balozi: Mwezi Aprili mwaka huu, Rais Xi na rais wa Zimbabwe walikuabliana kuboresha uhusiao kati ya mataifa haya mawili. Kabla ya haya, uhusiano wetu bado ulikuwa mzuri, na utaendelea kuimarika kila siku. Kadri siku zinavyosonga, ndivyo mahusiano pia yanazidi kubadilika. Hatujawahi kuwa na wakati ambao uhusiano baina yetu ulikuwa wa uzushi. Tuko sawa kabisa. Tunajali maslahi ya kila mmoja wetu. Sisi hapa Zimbabwe tunafahamu kuwa kuna China moja pekee duniani. China imekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za kibanadamu.

  Mwanahabari: Miaka 40 imepita tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguzi mlango. Wakati ukae hapa China kwa miaka 19, ni mabadiliko gani makubwa ya maisha yako ambayo umewahi kushuhudia?

  Balozi: Kiwango na juhudi za kupunguza umaskini katika taifa hili kubwa na kulingana na makadirio mbalimbali China itaondoa umasikini wote kabla ya muda uliopangwa. Moja ya takwimu ambazo ninazisoma na ninaamini ni za kweli ni kwamba kila mwaka China huondoa watu milioni 30 kutoka kwa umaskini. Watu milioni thelathini ni karibu idai ya watu wote wa Zimbabwe na hilo ni jambo la kupendeza. Karibu miaka 20 iliyopita au wakati China ilianza sera kufungua mlango na mageuzi ilikuwa kwenye nafasi ya 15 duniani kwa ukubwa wa kimapato na uchumi na sasa Chinaiko katika nafasi ya 2 na bado inakua kiuchumi. Kwa hiyo takwimu hizi mbili zinaelezea hadithi na ni hadithi tunayosherehekea. Maoni yangu kwa ujumla ni kwamba sera za kufungua mlango na mageuzi zilizoanzishwa na Deng Xiaoping zimeendelea kufanikiwa. Sasa ni fursa ya nchi nyingine duniani kote kuona ushirikiano na fursa ambapo kufanya kazi pamoja na China tunaweza wote kufaidika na kuwa na dunia bora zaidi kuliko ilivyokuwa.

  Mwanahabari: Unaonaje juu ya majukumu ya China kwa utulivu, usawa na ustawi wa uchumi wa dunia?

  Balozi: Takriban asilimia 30 ya pato la dunia linatoka China, ambalo ni mojawapo ya mataifa yanayoongoza kwa biashara duniani. Vile vile China ni miongoni mwa mataifa yanayoongoza kwa uzalishaji wa bidhaa mbali mbali. China imewekeza katika mataifa mengi duniani ili kuinua uchumi wake na wa mataifa mengine. Kando na haya, China inachangia sana ukuaji wa sekta ya utalii. Hivi karibuni wachina zaidi ya milioni 120, watakuwa wakitalii mataifa mengi ulimwenguni. Haya yote ni dhihirisho tosha kuwa China inachangia pakubwa sana. Miaka miwili iliyopita, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) liliifanya rmb kuwa mojawapo ya sarafu zinazotambulika duniani. Sarafu ya China rmb ni ya tatu kwa thamani kwenye sarafu ulimwenguni. Mataifa mengi sana , mengine kutoka Afrika yanatumia sarafu ya China. Ni matumaini yangu kuwa siku za mbeleni, taifa la Zimbabwe litatumia sarafu hii kama mojawapo ya fedha za kigeni.

  Mwanahabari: Kabla ya ziara yake nchini China mwezi Aprili, Rais Mnangagwa alisema kuwa kipaumbele chake cha utawala ni kufufua uchumi na kufanya Zimbabwe kufikia kipato cha katikati mwaka 2030, ambayo inahitaji uhusiano wa kina na China. Je, tunafanana katika pande gani tukijitahidi matokeo mazuri ili kuwasaidia watu wa nchi zetu mbili?

  Balozi: Sisi ni watu ambao hatungependa kuwa mahali ambako hatuwezi kunufaishana, sisi ni watu ambao hatupendi kunufaika wakati mwenzetu anaumia. Sisi pia ni watu ambao tunapenda kufanya mabadilishano kwa njia ya haki. Haya ndio mambo ambayo nimeyaona kwa China. China ni nchi muhimu sana hasa kwa ukubwa na idadi ya watu lakini hakuna siku utaiona ikitaka kukalia nchi zingine. Utakumbuka kuwa mwaka jana, rais Xijinping alizindua tunachokiita Uhusinao wake wa kidiplomasia na nchi za nje ambao unatambua umuhimu wa dunia kwa kila mmoja. Kwa hiyo kama raia wa Zimbabwe, ninaweza kusema kuwa mambo ambayo nayathamini sana moyoni mwangu ni wakati dunia inatoa fursa sawa iwe ni kwa nchi kubwa au ndogo. Kwa hiyo una uhusiano ambao umejengwa kwa misingi ya kuheshimiana na lengo ni kuifanya dunia kuwa nzuri zaidi.

  Mwanahabari: Sera ya China kwa Afrika zimetekelezwa kwa njia ya FOCAC na Ushirikiano na Ukanda Mmoja na Njia Moja, na kadhalika. Je, unaonaje sera za China kwa Afrika?

  Balozi: Natokea nchini Zimbabwe ambako aliyekuwa rais wetu Robert Mugabe alisema miaka 20 iliyopita wakati tulikuwa na shinikizo kubwa kutoka nje kuwa tuangalie kusini na kuangalia kusini inamaanisha kuimarisha uhusiano wetu na hii nchi muhimu sana iitwayo China. Wakati rais Xijinping alipokuja Afrika kwenye mkutano wa FOCAC mjini Johannesburgh, alikuwa amefanya ziara ya kitaifa nchini Zimbabwe na wakati huo rais wetu alikuwa Robert Mugabe. Mugabe alisema China inafanya kazi ambayo tulitarajia ingefanywa na nchi ambazo zilitukoloni lakini hazifanyi. Kwa hiyo matarajio yetu ni kuwa nchi zilizotukoloni zinatakiwa kujifunza kutoka kwa China kazi nzuri inayofanya , kazi ambayo rais Xijinping anafanya na alimalizia kwa kusema Mungu aibariki China na mungu ambariki rais Xijinping. Alikuwa anazungumza kutoka Moyoni. Haikuwa hotuba ambayo ilikuwa imeandaliwa. Na kwa uhakika tunasherehekea nchi ya Burkinafaso kwa kujiunga katika jamii ya kidiplomasia na China. Maoni yangu ni kuwa tuko mahali pazuri sana.Nilipokuja hapa miaka 18 iliyopita kulikuwa nan chi nyingi sana ambazo zilikuwa na uhusiano wa kidiplomasia nan chi zingine.

  Mwanahabari: Una matarajio gani juu ya FOCAC utakaofanyika hapa Beijing mwezi Septemba?

  Balozi: Nilipoanza kazi za uanadiplomasia mwaka 1999 biashara kati ya China na Afrika ilikuwa chini ya dola bilioni 10 lakini sasa tunazungumzia zaidi ya dola bilioni 200. Biashara kati ya pande hizo mbili imeongezeka mara 46 na hii ina maana fursa kwa watu pia imeongezeka kwa Kwa kiasi sawa na hicho. Hiyo ina maana kwamba wana chaguo zaidi na kuwepo na machaguo zaidi ndio tunayohitaji duniani. Kwa hivyo nina hisia nyingi nzuri kuelekea mkutano wa wa kilele wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika mwezi Septemba. Kama mikutano iliopita pia wakati huu China na Afrika watakuwa na sababu ya kusherehekea. Tunaangalia maslahi ya pande mbili lakini pia na maslahi ya pande zaidi ya mbii na nina uhakika na hekima ya rais Xi Jinping na utawala wake na chama cha CPC matunda ya mkutano huo yatakuwa mazuri kama vile tumekuwa tukishuhudia. Nchini Zimbabwe mwezi Septemba maua ya mti wa Jacaranda yanachanua kwa rangi ya zambarau.Itakuwa ni mahadhari ya kupendeza wakati huo. Naona mahadhari ya maua ya Jacaranda kama ishara ya kuwa na mkutano wenye fanaka wa FOCAC.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako