• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yatarajia mkutano ujao wa FOCAC wa Beijing uimarishe mafanikio ya ushirikiano kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-08-22 06:33:28

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia Bw Meles Alem amesema serikali ya Ethiopia inatarajia Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano wa China na Afrika FOCAC utakaofanyika mwezi ujao mjini Beijing utazidi kuimarisha mafanikio ya ushirikiano kati ya China na Afrika. Bw Meles ameisifu China kwa kuzipatia nchi za Afrika msaada kwa miaka mingi. Amesema,

    "Ushirikiano kati ya China na Afrika ni wa kunufaishana, China inaheshimu uhuru wa kisiasa wa nchi za Afrika, na kuzipatia msaada bila ya masharti. China ina nguvu kubwa ya ushawishi wa kisiasa duniani kote, na uchumi wake unachukua nafasi ya pili duniani, kwa hiyo China itaipatia Afrika msaada mkubwa katika maendeleo yake."

    Bw Meles pia amesema kwamba pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" la China linasaidia kuzidi kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika. Uwekezaji wa China kwenye ujenzi wa miundombinu ya Afrika unatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi za Afrika, ambazo ujenzi wa miundombinu barani Afrika unahitaji msaada wa China. Hivi sasa kiasi cha uwekezaji kutoka China katika miradi ya Ethiopia kimefikia dola bilioni 4 za kimarekani, pia China imeipatia Ethiopia teknolojia na fedha kwa ajili ya kuimarisha ujenzi wa miundombinu na sekta ya nishati. Serikali ya Ethiopia inatumai kuwa mkutano wa kilele wa mwaka huu utaweza kuimarisha zaidi mafanikio yaliyopatikana kwenye ushirikiano kati ya China na Afrika ikiwemo Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako