• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhusiano wa Burundi na China watajwa kuingia kwenye kipindi kizuri zaidi katika historia

    (GMT+08:00) 2018-08-22 10:21:46

    Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Bw Alain Aime Nyamitwe amesema Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano wa China na Afrika FOCAC utakaofanyika mwezi Septemba mjini Beijing utasaidia kuimarisha uhusiano kati ya Burundi na China, na kuhimiza maendeleo ya Burundi.

    Bw Nyamitwe amesema kuwa huu ni mwaka wa 53 tangu Burundi na China zilipoanzisha uhusiano wa kibalozi, na uhusiano huo umeingia kwenye kipindi kizuri zaidi katika historia. Amesema Burundi inapenda kuendelea kuimarisha ushirikiano na China kwenye nyanja mbalimbali.

    "Burundi inapenda kushirikiana na China kwenye sekta nyingi, na kuiunga mkono China kufanya mkutano wa kilele wa FOCAC. Katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika uliofanyika mwaka huu, nchi za Afrika zimekubaliana kwa kauli moja kuwa China ni rafiki mkubwa wa Afrika, ambayo inaweza kutoa msaada mkubwa kwa maendeleo ya Afrika."

    Bw Nyamitwe pia amesema kitabu cha "Utawala wa Nchi" kinachoandikwa na rais Xi Jinping wa China kina ushawishi mkubwa nchini Burundi. Amehifadhi matoleo ya lugha za kireno, kifaransa na kiingereza ya kitabu hicho, na kupata mengi ya kujifunza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako