• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa Rwanda nchini China aeleza ushirikiano kati ya China na Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-08-23 08:37:39

    "Katika makumi ya miaka iliyopita, China na Afrika zimeshirikiana na kushikamana kwa dhati. Zinadumisha hali ya kuwa jumuiya yenye hatma na maslahi ya pamoja." hayo yamesemwa na rais Xi Jinping wa China wakati alipotembelea Afrika mwezi Juni, mwaka huu. Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika. FOCAC utakaofanyika hivi karibuni, unafuatiliwa sana duniani. Kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo, waandishi wa habari wa CRI wamefanya mahojiano na mabalozi wa Tanzania, Zimbabwe, Rwanda, Uganda, Burundi na Afrika Kusini nchini China, kuhusu mafanikio na maendeleo yaliyopatikana chini ya mfumo wa FOCAC, kuhimiza ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja ili kupata maslahi ya pamoja ya China na Afrika. Hivi karibuni tumemhoji balozi wa Rwanda nchini China Bw. Charles Kayonga akieleza ushirikiano kati ya China na Rwanda.

    Mwanahabari: Miaka 40 imepita tangu China ianze kutekeleza sera za mageuzi na ufunguzi mlango. Ni mabadiliko gani makubwa ya maisha ambayo umewahi kushuhudia ukikaa hapa China?

    Balozi: China kujihusisha na bara la Afrika kunakaribishwa sana kwa sababu tunahitaji fedha kuanzisha viwanda na tunahitaji fedha kujenga miundombinu. China inaleta pesa kwenye benki zetu au kwenye bara letu, tunafanya biashara na pande zote zinanufaika na zinaungana. China inakuwa nchi ya matumizi tangu rais Xi Jinping alivyoanza mageuzi haya akijikita kwenye uwekezaji mkubwa katika miundombinu kwenye uchumi ambao ni wa matumizi na wa huduma. Uchumi utaungana zaidi. China inatumia malighafi nyingi kutoka Afrika, Afrika inapokea mtaji kutoka China, na hii ndio ile tunaita ushirikiano wa kunufaishana.

    Mwanahabari: Viongozi wa nchi 14 za Kusini na Mashariki ya Afrika wamehudhuria baraza na kukubali juu ya utumiaji wa Yuan ya China kama fedha za akiba kwa kuwa China kufanya kazi muhimu katika uchumi wao. Je! Unaona uwekezaji wa China katika sekta ya kifedha barani Afrika kupitia mabenki ya China, vipi China inaimarisha uchumi wa Afrika?

    Balozi: Nilipokuja hapa mara ya kwanza mwaka 1995 na nilivyoletwa hapa miaka minne iliyopita nimeona mabadiliko dhahiri yaliyoathiri maisha ya watu. GDP ya China imebadilika kutoka wakati wa mageuzi na kufungua mlango mwaka 1978 ilikuwa chini ya dola 300 za kimarekani na leo ni dola 7000 hivi za kimarekani, na unaweza kushuhudia hili unapotembelea maduka makubwa na kuona watu wakifanya manunuzi, barabarani unaweza kuona ongezeko la magari watu wanaendesha. Nilipokuja mwaka 1995 watu walikuwa wanaendesha baskeli. Ongelea treni za kasi, ongelea urahisi ulioletwa na teknolojia ya mawasiliano, watu wa kawaida wanafanya biashara kwenye internet, na hata kufanya mawasiliano ya kawaida kupitia wechat na mitandao mingine ya kijamii. Athari ya mabadiliko haya imekuwa dhahiri na imerahisisha maisha ya watu. Na unaweza kuona Wachina wana furaha. Mabadiliko chanya ya China yanaweza pia kuathiri Afrika, kwa sababu China imekuwa tajiri unaweza kuona kuongezeka kwa biashara zake barani Afrika.

    Mwanahabari: Sera za China kwa Afrika zimetekelezwa kwa njia ya FFOCAC na Ukanda Mmoja na Njia Moja. Je! Una matarajio gani juu ya mkutano wa FOCAC ujao utakaofanyika hapa Beijing mwezi Septemba?

    Balozi:Rwanda kwa ujumla ni nchi inayovutia. Mandhari, milima, kaskazini na magharibi, hifadhi za volcano kaskazini mwa Rwanda na hapo ndipo utaweza kuwaona Nyani wa milimani. Unaweza kutembelea na kuona familia za Nyani na hata kuwasiliana nao na kuketi nao na kama kuzungumza nao vile. Nimewaona watalii kutoka China waliokwenda pale na kugusana na Nyani wa milimani. Wanasema jeni zao ni kama asilimia 99 ya zile za binadamu na hivyo, ni uzoefu mzuri kwa hakika ni mara moja katika maisha hivyo nawashawishi Wachina kwenda kule.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako