• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia kuchukua hatua za kukabiliana na vikwazo vilivyowekwa na Marekani

    (GMT+08:00) 2018-08-23 17:00:15

    Rais Vladmir Putin wa Russia amesema vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Russia havina maana, na vinakwenda kinyume na matarajiao ya Marekani. Tangu Marekani ilipotangaza kuweka vikwazo dhidi ya Russia mwanzoni mwa mwezi huu, Russia imechukua hatua mbalimbali ili kukabiliana na hali hiyo.

    Marekani tarehe 21 ilitangaza duru mpya ya vikwazo dhidi ya Russia, ambavyo vinalengea mashirika, watu binafsi na meli kadhaa za Russia kutokana na vitendo vibaya kwenye mtandao wa Internet, kusaidia mashirika yaliyowekewa vikwazo na Marekani, na kutoa mafuta safi kwa meli yenye bendera ya Korea ya Kaskazini. Kabla ya hapo, wizara ya mambo ya nje ya Marekani mwanzoni mwa mwaka huu ilisema, Marekani inahakika kuwa Russia ilikwenda kinyume na sheria ya kimataifa katika tukio la jasusi wake wa zamani kutiliwa sumu kwenye chakula nchini Uingereza, na imeamua kuweka vikwazo dhidi ya Russia ikiwemo kupiga marufuku kuuza bidhaa na teknolojia nyeti zinazohusika na usalama wa taifa kwa Russia.

    Ili kukabiliana na vikwazo vilivyowekwa na Marekani ambavyo vinaathiri vibaya uchumi wa Russia, Russia imechukua hatua mbalimbali. Hatua ya kwanza ni kuongeza ushirikiano na Iran, Uturuki na hata baadhi ya nchi marafiki wa Marekani. Mwezi huu, licha ya Russia, Marekani kwa nyakati tofauti pia iliweka vikwazo dhidi ya Iran na Uturuki. Baada ya Marekani kurejesha vikwazo dhidi ya Iran, Russia ilitangaza kudumisha ushirikiano wa uchumi na biashara na Iran. Tarehe 13 mwezi huu, waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Lavrov alifanya mazungumzo na mwenzake wa Uturuki Bw. Mevlut Cavusoglu, na kulaani Marekani kwa kauli moja, wakisema vikwazo vya Marekani havitaathiri ushirikiano kati ya Russia na Uturuki. Wakati huo huo, rais Putin wa Russia tarehe 18 baada ya kushiriki kwenye harusi ya waziri wa mambo ya nje wa Austria, alifanya mazungumzo na chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel.

    Hatua ya pili ni kupunguza mali za dola za kimarekani. Waziri wa fedha wa Russia Anton Siluanov hivi karibuni alisema, Russia imepunguza mali zinazohesabiwa kwa dola za kimarekani kwa kiasi kikubwa zaidi. Takwimu zilizotolewa na wizara ya fedha ya Marekani zinaonesha kuwa, kuanzia mwezi Machi hadi Mei mwaka huu, dhamani za Marekani zilizomilikiwa na Russia zimepungua na kuwa dola za kimarekani bilioni 14.9 kutoka 96.1.

    Hatua ya tatu ni kujitahidi kujenga uhusiano wa kiwenzi na nchi za Ulaya na Asia. Mwezi Mei mwaka 2016, kwenye kongamano la kimataifa kuhusu mambo ya uchumi lililofanyika mjini St. Petersburg, rais Putin alitoa wito wa kujenga umoja wa kiuchumi wa kushirikisha Russia, Umoja wa Ulaya, India, China, na nchi nyinginezo. Wasomi wengi wa Russia wanaona katika miaka ya hivi karibuni kutokana na mabadiliko ya hali ya kimataifa na kikanda, haswa marekebisho ya sera za Marekani, mpango wa kujenga umoja huo una maana zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako