• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele wa FOCAC watarajiwa kuinua kiwango cha ushirikiano kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-08-24 09:14:27

    Balozi wa China nchini Ethiopia Bw Tan Jian amesema Mkutano wa kilele wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utakaofanyika hivi karibuni mjini Beijing unatarajiwa kuinua kiwango cha ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Mkutano huo wa kilele utafanyika tarehe 3 na 4 Septemba mjini Beijing, ukiwa na kaulimbiu "China na Afrika: kuelekea jumuiya imara zaidi yenye hatma ya pamoja kwa kupitia ushirikiano wa kunufaishana".

    Bw Tan Jian amesema mkutano huo utawapatia viongozi wa China na nchi za Afrika fursa ya kujadiliana na kuweka mipango ya makini kwa pamoja katika ushirikiano kati ya China na Afrika. Amesisitiza kwamba mkutano huo utaweka jukwaa muhimu la kuhimiza ushirikiano wa kirafiki wa pande zote kati ya China na Afrika, na kukabiliana na changamoto ya kimataifa inayozikabili, ili kuzidi kuhimiza maendeleo ya nchi zinazoendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako