• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China ahimiza juhudi za kuendeleza maeneo ya magharibi mwa China

    (GMT+08:00) 2018-08-24 09:29:14

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa wito wa juhudi zaidi kufanywa kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya watu katika sehemu za magharibi mwa China.

    Bw. Li ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kudumu ya ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China CPC, na mkuu wa kikundi cha uongozi wa maendeleo ya sehemu za magharibi cha baraza la serikali, pia amesema sehemu ya magharibi inatakiwa kuendelea na mageuzi na ufunguaji mlango, na kuhimiza uvumbuzi ili kutimiza maendeleo yenye ubora wa juu.

    Bw. Li ameyataja maendeleo ya sehemu za magharibi kama hatua muhimu na ngumu kwa China kuwa na jamii yenye maisha bora na kutimiza mambo ya kisasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako