• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Uganda akagua ujenzi wa kituo cha umeme wa maji unaofadhiliwa na China

    (GMT+08:00) 2018-08-24 09:46:42

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekagua ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa nguvu za maji cha Karuma unaofadhiliwa na China, ambacho ni kituo kikubwa zaidi cha umeme cha aina hiyo nchini Uganda.

    Wakati wa ukaguzi huo, rais Museveni ameishukuru serikali ya China kutokana na mikopo yake mikubwa kwa ajili ya mradi huo.

    Waziri wa maendeleo ya nishati na madini Bibi Irene Muloni amesema ujenzi huo unaoendelea kwa miaka mitano, utakamilika mwishoni mwa mwaka ujao. Balozi wa China nchini Uganda Bw. Zhang Zhuqiang amemshukuru Rais Museveni kwa uungaji mkono wake, na kusema kuwa mradi huo ni alama ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Uganda ambao umewaajiri waganda zaidi ya 6,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako