• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asimulia hadithi kuhusu wanandoa wa China kwenda Tanzania kwa ajili ya fungate

    (GMT+08:00) 2018-08-24 17:41:11

    Rais Xi Jinping wa China, ambaye ameongoza katika mapambano dhidi ya ufisadi na kuendeleza mageuzi, pia ni hodari sana wa kusimulia hadithi. Wakati akiongea kwenye mikutano, kwenda sehemu mbalimbali kufanya utafiti na ukaguzi, kutoa hotuba alipofanya ziara, au kutoa makala kwenye magazeti, anapenda kusimulia hadithi kueleza wazo lake na kuwatia moyo watu wengine. Hadithi hizo zinaonyesha busara ya China na nguvu ya China, pia zinaonyesha hisia za utamaduni na undani wa filosofia ya rais Xi, na kusimulia hadithi kumekuwa umaalumu wa mtindo wake wa uongozi.

    Mwezi Machi mwaka 2013, baada ya kuwa rais wa China, rais Xi Jinping alichagua Tanzania kuwa kituo chake cha kwanza katika ziara yake barani Afrika. Tarehe 25, Machi, rais Xi Jinping alipohotubia kwenye kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere, alisimulia hadithi kuhusu vijana wa China wanavyotamani Afrika, wanavyosafiri Afrika na wanavyoipenda Afrika.

    "Niliwahi kusikia hadithi moja iliyoeleza kuwa, kuna wapenzi vijana wa China, ambao waliifahamu Afrika kupitia vipindi vya televisheni walipokuwa watoto, hivyo walikuwa na shauku kubwa kwa Bara la Afrika. Baadaye walioana, wakaenda Tanzania kwa ajili ya fungate. Katika siku ya kwanza ya wapendanao baada ya kuoana, walifunga safari ya kwenda Tanzania, na kujionea mila na desturi za watanzania na mandhari nzuri ya Hifadhi ya Serengeti. Baada ya kurudi China, waliandika waliyoyaona nchini Tanzania kwenye ukurasa wao wa mtandao wa kijamii, na kusomwa na maelfu ya watu na kupata mamia ya maoni kwenye mtandao wa kijamii. Wamesema, kweli wameipenda Afrika, na mioyo yao haiwezi kuondoka tena kwenye bara hilo lenye miujiza."

    Hadithi hiyo inaonyesha hisia ya watu wa China kwa Afrika, na hiki ni kipindi cha kisasa kwenye historia ya mawasiliano ya urafiki kati ya China na Afrika. Rais Xi pia ni shuhuda wa urafiki kati ya China na Afrika. Aliwahi kwenda Afrika mara tisa. Hadithi aliyosimulia inaonyesha watu wa China na Afrika wana hisia ya karibu, kuimarisha mawasiliano kati ya watu ndipo urafiki kati ya China na Afrika utazidishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako