• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuishi pamoja na mkonge

    (GMT+08:00) 2018-08-25 16:05:57

    Mwezi Desemba mwaka 2015, Rais Xi Jinping wa China alitoa taarifa katika mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika Johannesburg kuwa China itazidisha zaidi uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote na Afrika. Rais Xi alisema Mipango kumi ya Ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye sekta ya viwanda, kilimo cha kisasa, miundo mbinu, uchumi, maendeleo yasiyosababishab uchafuzi, uwekezaji na biashara, kupunguza umaskini, afya, utamaduni, amani na usalama yamefungua mlango mpya wa uhusiano kati ya China na afrika.

    Wakati mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika unakaribia kufanyika mjini Beijing tunafuatilia Mipango kumi ya Ushirikiano kati ya China na Afrika, na kuona jinsi uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Afrika unavyozidi kukua. Tunaanza kuhusu kuishi pamoja na mkonge.

    Asubuhi ya Jumapili, katika kijiji kimoja kidogo kilichoko karibu na mji wa Morogoro, watu wote bado wamelala. Lakini mchina mmoja mwenye umri wa miaka 65, Wan Lusheng ameamka mapema kama kawaida, kwenda kwenye kiwanda na mashamba ya mkonge. Hadi sasa Amefanya kazi hiyo kwa miaka 20.

    Mwaka 1999, mtaalamu wa kilimo Bw. Wang Lisheng alijiunga na Kampuni ya Kilimo ya China kusaidia ujenzi na uendeshaji wa Shamba la mkonge la Morogoro, kusukuma mbele maendeleo ya kilimo kwa njia ya ushirikiano. Shamba hili lilikuwa limetelekezwa kabla ya kuchukuliwa na kampuni ya Kilimo ya China. Mmiliki wa shamba hilo alichagua kampuni ya China kwa sababu aliamini kuwa wachina wanaweza kuendeleza shamba hilo vizuri, na kwa sababu ya urafiki mkubwa kati ya China na Afrika. Alitumai kuwa wachina wanaweza kuokoa ardhi hiyo na kusaidia maendeleo ya kilimo cha Tanzania. Bw. Wang Lusheng na wafanyakazi wenzao waliamini kuwa hawezi kushindwa amani ya watu wa Tanzania. Lakini mwanzoni walikabiliana na matatizo mengi, kwa kuwa shamba hilo lilitelekezwa kwa muda mrefu, na vichaka vilijaa kila mahali.

    "Tulipokuwa tunalima, shamba lilikuwa limejaa vichaka, na vyote vilikuwa vikubwa, kwa hivyo tulikuwa na kazi ngumu ya kulima wakati ule."

    Muda ya kukua kwa mikonge ni takriban miaka mitatu. Kutoka kupanda miche hadi kuuza mikonge iliyokomaa itachukua muda mrefu zaidi. Bw. Wang Lusheng alifanya kazi kwa bidii kabisa na kukabiliana na matatizo mengi. Hakuwa na mashine za kusafirisha maji taka, Bw. Wang alitengeneza mashine mbili yeye mwenyewe. Mkonge haupendi maji mengi, lakini shamba hilo liko kwenye eneo tambarare, na kila msimu wa mvua maji yanatuama kila mahali, Bw. Wang alilazimiska kutumia njia za jadi za china kutatua tatizo hilo. Hatimaye Bw. Wang Lusheng na wafanyakazi wenzake walipita muda mgumu, baada mwaka 2005 shamba hilo lilianza kupata mapato, wataalumu wote wa China walifurahi sana.

    "Tulianza kupanda mikonge mwaka 2005, na mwaka 2006 tulianza kupata mapato. Hadi mwaka 2011 kiasi cha uzalishahji wetu kimefikia tani 2000 kila mwaka.Baada mwaka 2011, bidhaa zetu ziliboreshwa na zaidi ya asilimia 80 zilifikia kiwango cha UG, na bei ya bidhaa hizo zimeongezeka. Shirikisho la Mikonge la eneo hilo lilitupongeza sana."

    Mwanzoni mwa Karne ya 21, kutokana na matumizi nyuzi mpya za sanisia, "nchi ya mikonge" Tanzania haikupata fursa nzuri ya kuendeleza kilimo cha mkonge. Kilimo cha mkonge kiliathirika sana. Wakati huo huo Shamba la Mikonge la Kampuni ya Kilimo cha China liliweza kujiendeleza, jambo hilo lililetea Tanzania mapato mengi ya fedha za kigeni.

    "Tulipofika Tanzania, kulikuwa na mashamba machache sana ya mkonge. Kilimo cha mkonge hakikuwa na maendeleo makubwa. Wakati ule kiasi cha uzalishaji wa mkonge Tanzania kwa mwaka, kilikuwa ni tani 20,000 tu. Baada mwaka 2011, mkonge wetu ulianza kuuzwa kwenye soko la Marekani, kiasi cha uzalishaji wetu kwa mwaka kilifikia tani 2500, na kuiingizia Tanzania fedha nyingi za kigeni. Wakati ule Tanzania, hasa sekta ya kilimo ya Tanzania, haikuwa na fedha nyingi kutoka nje."

    Licha ya fedha zilizoletwa na shamba hilo, Kampuni hiyo ya China pia ilifanya maisha ya wenyeji wengi kuwa na mabadiliko makubwa.

    "Tulipofika hapa, vijiji vya kwenye eneo hili vilikuwa maskini sana, shamba letu ndio liliongeza nafasi nyingi za ajira kwa vijiji hivyo. Idadi ya wafanyakazi tulioajiri ilifikia 1000. Wafanyakazi hao wote waliishi hapa, kwa hiyo eneo hilo lilipata fursa nzuri ya kuendeleza uchumi. Mapato ya wenyeji yaliongezeka, na kuweza kununua mbegu, kwa hiyo watu wengi walianza kulima, na kilimo kilipata maendeleo vilevile."

    Shamba la Kampuni ya China lilijenga pampu ya maji ya bomba na zahanati kwa ajili ya kijiji hicho. wanakijiji wote sasa wanaweza kunywa maji safi, na hawahitaji kusafiri mbali sana kwa ajili ya kupata matibabu.

    "Shamba letu lilikkisaidia kijiji cha Peyapeya kupata maji ya kunywa. Tuliweka bomba kati ya kisima cha shamba na kijiji. Tulifikiri kampuni yetu inapaswa kuwaletea wenyeji manufaa fulani. Tulifanya kazi nyingi kutimiza lengo hilo."

    Mfanyakazi Majaliwa na familia yake walihamia kwenye mabweni ya wafanyakazi hivi kiaribuni. Shamba lilikuwa mbali na vijiji, kwa ajili ya kutatua tatizo hilo, mwaka 2017 shamba lilijenga majengo mengi ya makazi kwa ajili ya wafanyakazi. Kulikuwa na sebule, vyoo na vyumba vya kulala. Tulipozumgumza kuhusu nyumba mpya, mke wa Bw Majaliwa, Bibi Olivia alikuwa na furaha sana.

    "Nyumba yetu mpya ni nzuri, shamba lilitusaidia sana. Tunaweza kuishi kwenye nyumba nzuri kama hiyo, tunapata umeme pia. Hatuhitaji kutoa pesa, na tunapata mshahara kama kawaida. Tunashukuru sana."

    Shamba pia lilitoa fursa ya kwenda China kujifunza kwa wafanyakazi. Bw. Majaliwa amekwenda China mara 3, aliona mabadiliko yanayoletewa na shamba la China kwa macho yake mwenyewe.

    "Kwanza ninataka kushukuru kampuni ya China inatupa mshahara kwa wakati. Nilipofanya kazi kwenye shamba lingine, baadhi ya wakati sikuweza kupata mshahara kwa miezi miwili. Mwanzoni wafanyakazi wote wa shamba hawakuwa na baiskeli, sasa wengi wamepata baiskeli, hata baadhi ya wafanyakazi walipata pikipiki au magari. Shamba limeleta mabadiliko kwenye maisha yetu. Zamani hakuwa na duka hapa kijijini, lakini sasa tuna maduka mengi sana. Hii ni kwa sababu mapato yetu yameongezeka na tumepata uwezo wa kununua vitu."

    Shamba limepata maendeleo makubwa, uchumi wa eneo hilo pua unasongea mbele. Lakini Bw. Wang Lusheng na wafanyakazi wenzake hawajivunii. Mzunguko ni muhimu sana kwa maendeleo ya kilimo, mazingira ya Tanzania ni mazuri sana kwa kilimo cha mkonge, na shamba linataka kufanya mambo mengine mazuri kwa ajili ya mazingira. Sasa shamba lilinunua mashine zinazoweza kuondoa maji taka na takataka za uzalishaji. Shamba lilitumia takataka hizo kama mbolea, na linakusanya maji taka kwa ajili ya kuzalisha umeme.

    "Maji taka na takataka za uzalishaji vina harufu mbaya. Tunaondoa maji na takataka kwa ajili ya kuumia bora. Maji taka yanaweza kuzalisha gesi. Kiasi cha methane inayozalishwa na mashine hiyo kinaweza kuendesha jenereta moja ya wati 150,000. Pia saponin ndani ya maji ya mkonge inaweza kutumika kwenye sekta ya afya. Takataka za uzalishaji za mkonge pia ni aina moja nzuri ya mbolea."

    Viwanda vinaendelea vizuri duniani, matumizi ya mkonge kwenye utengezaji wa madaraja na kamba za lifti unakuwa muhimu zaidi. Mahitaji ya mkonge kwenye soko la duniani yameanza kuongezeka. Bw. Wang Lisheng anafikiri kilimo cha mkonge nchini Tanzania kina fursa nzuri, lakini pia kinakabiliwa na matatizo.

    "Nafikiri sasa ni fursa nzuri sana, Tanzania ina mazingira mazuri sana, na pia ina idadi kubwa ya mkonge wa zamani, kilimo cha mkonge cha Tanzania kitapata maendeleo makubwa. Sasa kiasi cha uzalishaji wa mkonge nchini Tanzania kwa mwaka kimefikia tani 30000 tu, Lakini zamani kilikuwa tani zaidi ya tani 200,000.Kuna changamoto nyingi, kwanza ni ukosefu wa mitaji, pili ni uzalishaji wa nyuzi za majani ya mkonge. Tumetatua matatizo hayo mawili nchini China, sasa tunatafuta njia ya kusaidia Tanzania kuendeleza kilimo hicho."

    Kuisaidia Afrika kuendeleza uwezo wa kuzalisha bidhaa za kilimo, na kuongeza thamani za bidhaa zinazouzwa nje, ni sehemu muhimu kwenye ushirikiano kati ya China na Afrika. Meneja mkuu wa Kampuni ya Kilimo ya China Bw. Bao Feng amesema kampuni hiyo imefanya utafiti kuhusu mashine kwa ajili ya kusaidia Tanzania kwenye eneo la uzalishaji wa bidhaa za kilimo cha mkonge.

    "Sasa tunafanya majaribio. Mashine za aina hiyo ni mashine nzuri sana nchini China, pia ni mashine za hali ya juu duniani. Lakini hatujui kama zinaweza kuendeshwa vizuri Afrika. Tunatarajia mashine za aina hiyo zinaweza kutumika. Halafu tunaweza kufanya ushirikiano na kampuni za Tanzania, na kuongeza uwezo wa kuzalisha bidhaa za kilimo nchini Tanzania."

    Sasa eneo lenye mkonge kwenye shamba hilo limefikia hekta 2000, na baadaye litaongezeka. Bw Wang Lusheng na wafanyakazi wenzake wanaona ardhi hiyo inapata maendeleo. Bw. Wang ana umri wa miaka 60 sasa, hajui atafanya kazi hiyo kwa muda gani, lakini amesema ataikumbuka ardhi hiyo daima.

    "Nina furaha sana kila siku ninaweza kufanya kazi za kawaida hapa. Niliona shamba hilo likipata maendeleo. Hata kama siku moja nitaondoka, nitaikumbuka ardhi hii na kujali maendeleo ya shamba letu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako