• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa Uganda nchini China aeleza ushirikiano kati ya China na Uganda

    (GMT+08:00) 2018-08-25 16:10:34

    "Katika makumi ya miaka iliyopita, China na Afrika zimeshirikiana na kushikamana kwa dhati. Zinadumisha hali ya kuwa jumuiya yenye hatma na maslahi ya pamoja." hayo yamesemwa na rais Xi Jinping wa China wakati alipotembelea Afrika mwezi Juni, mwaka huu. Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika. FOCAC utakaofanyika hivi karibuni, unafuatiliwa sana duniani. Kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo, waandishi wa habari wa CRI wamefanya mahojiano na mabalozi wa Tanzania, Zimbabwe, Rwanda, Uganda, Burundi na Afrika Kusini nchini China, kuhusu mafanikio na maendeleo yaliyopatikana chini ya mfumo wa FOCAC, kuhimiza ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja ili kupata maslahi ya pamoja ya China na Afrika. Hivi karibuni tumemhoji balozi wa Uganda nchini China Bw. Chrispus Kiyonga akieleza ushirikiano kati ya China na Uganda.

    Mwanahabari: Ushirikiano kati ya China na Uganda umeboreshwa mwaka kwa mwaka na tuna uhusiano mzuri na ushirikiano katika maeneo kama vile Viwanda.

    Balozi: Naweza kusema mojawepo wa maeneo bora zaidi ya ushirikiano wetu katika uchumi, kwanza ni uzalishaji wa kawi. Kupitia ushirikiano wetu wa China na Uganda tumezalisha karibu mara mbili ya kawi yetu. Vituo viwili vya umeme wa maji vilijengwa kwa ushirikiano na ufadhili wa China. Sasa china inachangia idadi kubwa zaidi ya uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja katika nchi yetu. Mwaka jana China ilikuwa muuza mkuu wa bidhaa nchini Uganda. Na pia sasa China ni mwezi wetu mkuu wa kimaendeleo.

    Mwanahabari: Je, unaonaje juu ya mafanikio ya uchumi wa China na mchango wake katika maendeleo ya kiuchumi kwa Bara la Afrika?

    Balozi: Kwa ndani ya mwaka mmoja nimetembelea mikoa saba au nane nje ya Beijing. Nimekuwa Guangdong zaidi ya mara tatu na moja ya mwisho ilikuwa mapema mwezi huu. Ushirikiano kati ya China na Afrika unaongezeka katika eneo la miundombinu, uwekezaji, watu kwa watu na nadhani katika awamu inayofuata tunaweza kufanya kazi zaidi kwa mauzo ya nje nchini China kutoka Afrika. Kutoka Uganda hasa tunataka kuuza nje bidhaa za kilimo na utalii. Tungependa marafiki wetu kutoka China kutembelea Afrika, kutembelea Uganda, Uganda ni sehemu ya kuvutia ya Afrika.

    Mwanahabari: Hivi karibuni serikali ya China inajaribu kuimarisha bidha za nje za Uganda kwa njia ya sera kadhaa ambazo hupenda ikiwa ni pamoja na kuondoa ushuru kwa asilimia 97 ya bidhaa, kwa hivyo Uganda itafaidikaje zaidi chini ya FOCAC?

    Balozi: Swala la kuuza nje bidhaa zetu ni muhimu sana na nadhani kwa kufuata uhusiano wetu wa kihistoria na urafiki na watu wa China tunapaswa kuboresha haraka mipango kwa sababu China ina soko kubwa la watu bilioni 1.3 wenye mafanikio makubwa ya kiuchumi. Kwa hiyo sisi marafiki wa China tunapaswa kushiriki katika mafanikio haya. China hadi sasa inaagiza karibu bidhaa za kilimo zenye thamani ya dola bilioni 120. Hivyo Afrika inapaswa kuwa na mgao wa soko hilo. Uganda ni nchi inayoongoza Afrika kwa kuuza nje kahawa na tunaongeza uzalishaji wetu wa kahawa na tunadhani katika miaka mitano ijayo uzalishaji wetu utaongezeka mara tano. Kwa sasa tunauza maembe na tunaweza kuongezeka, tunauza ufuta na tunaweza kuuza zaidi, tunaweza kuuza pia samaki na maua. Na sisi nchini Uganda tunahitaji teknolojia na mashine kutoka China na tunaweza pia kuwa na ubia pamoja na wakulima wetu ambapo tunaweza kuzalisha bidhaa za kilimo kusindika na kuleta hapa. Kwa hiyo suala hili la kuuza nchini China ni suala la kimkakati. Natumaini kwamba FOCAC ijayo mbali na mambo mengine pia itazingatia suala hili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako