• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa chama tawala cha Kenya atarajia mkutano wa FOCAC utaisaidia Kenya kutimiza ajenda ya Big Four

    (GMT+08:00) 2018-08-26 15:39:54

    Katibu mkuu wa chama tawala wa Jubilee cha Kenya Bw. Raphael Tuju amesema anatarajia kuwa Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utakaofanyika mwezi ujao mjini Beijing utaisaidia Kenya kutimiza ajenda yake ya Big Four iliyotolewa na rais Uhuru Kenyatta.

    Bw. Tuju amesema mjini Nairobi kuwa Kenya inatumai kuwa mkutano ujao wa FOCAC utapata matokeo halisi, na kuimarisha ushirikiano kati ya Kenya na China katika nyanja za kilimo, viwanda, ujenzi, ili kuisaidia Kenya kufikia malengo yake.

    "Kwa upande wetu, tunafuatilia zaidi ajenda ya Big Four aliyotoa Rais Uhuru Kenyatta wakati wa muhula wake wa pili. Kwa mfano wa suala la usalama wa chakula, tunatumai kuwa sekta binafsi za Kenya na China zitaweza kushirikiana katika kuimarisha usalama wa chakula. Wakati huo huo, pia tunatarajia kukuza ushirikiano na China katika sekta ya viwanda. Makampuni ya China yanajenga viwanda nchini Kenya, kuisaidia Kenya kuwa kituo cha viwanda cha Afrika Mashariki, na pia kutoa fursa za ajira kwa vijana wetu. Aidha, katika sekta ya ujenzi, China ikiwa ni nchi yenye idadi kubwa ya watu, imeendeleza teknolojia nyingi za hali ya juu zenye ufanisi mkubwa na gharama za chini, ili kukidhi mahitaji yake ya ndani, na haya pia ni mambo tunayotaka kujifunza kutoka kwa China. "

    Bw. Raphael pia ametolea mfano wa mradi wa Reli ya SGR ya Mombasa-Nairobi na kuisifu China kuleta fursa ya maendeleo kwa Kenya na Afrika kutokana na Pendekezo lake la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    "Reli ya Mombasa na Kenya ni faida wazi ya mpango wa Ukanda Mmoja Njia Moja uliotajwa na China. Katika miaka mia moja iliyopita hakukuwa na mradi kama reli hiyo kwenye kanda ya Afrika Mashariki. Kwa sasa, mradi huu bado uko kwenye hatua ya kwanza, kisha ukapanuliwa kuelekea Uganda, kupita Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC, na kufika Sudan na Sudan kusini. Muunganyiko huu wa Reli una umuhimu mkubwa kwa uchumi na maisha ya watu wetu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako