• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa Burundi nchini China aeleza ushirikiano kati ya China na Burundi

    (GMT+08:00) 2018-08-27 07:28:30

    "Katika makumi ya miaka iliyopita, China na Afrika zimeshirikiana na kushikamana kwa dhati. Zinadumisha hali ya kuwa jumuiya yenye hatma na maslahi ya pamoja." hayo yamesemwa na rais Xi Jinping wa China wakati alipotembelea Afrika mwezi Juni, mwaka huu. Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika. FOCAC utakaofanyika hivi karibuni, unafuatiliwa sana duniani. Kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo, waandishi wa habari wa CRI wamefanya mahojiano na mabalozi wa Tanzania, Zimbabwe, Rwanda, Uganda, Burundi na Afrika Kusini nchini China, kuhusu mafanikio na maendeleo yaliyopatikana chini ya mfumo wa FOCAC, kuhimiza ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja ili kupata maslahi ya pamoja ya China na Afrika. Hivi karibuni tumemhoji balozi wa Burundi nchini China Bw. Martin Mbazumutima akieleza ushirikiano kati ya China na Burundi.

    Mwanahabari: Burundi ni moja ya nchi ambazo zimenufaika na mpango wa China wa utekelezaji wa sera za maendeleo ya pamoja barani Afrika kupitia FOCAC tangu mwaka 2000. Pamoja na msaada wa dola za kimarekani milioni 164 iliopata Burundi kutoka serikali ya China, Je, kwa mtazamo wako, ni mambo gani unaweza kusema yanathibitisha hilo?

    Balozi: Kama mnavyosema Burundi imenufaika na mpango huo wa FOCAC ulioanza mwaka 2000, na kama mjuavyo Burundi ni nchi ambayo uchumi wake ungali mdogo sana,na kwa muda huu nchi haiwezi kupata mikopo kutoka kwenye mabenki, ila sasa China imeisaidia Burundi iwe na msukumo katika maendeleo yake. Msaada huo umetumika kwa maeneo mengi, kwenye majengo, masuala ya masomo, umesaidia pia kukuza kiwango cha kutoa habari, pamoja na kilimo. Msaada huo umesaidia Burundi na kama mjuavyo miaka iliyopita Burundi ilikuwa kwenye matatizo ya vita, ilikuwa hivyo ilikuwa muhimu ipate jinsi ya kuendeleza uchumi wake na jinsi ya kuweza kuishi bila matatizo.

    Mwanahabari: Kwa kuwa Ukanda wa Afrika Mashariki, ni moja ya maeneo muhimu ya Utekelezaji wa sera ya China ya kuimarisha mawasiliano na maendeleo ya kiuchumi na kibiashara duniani kupitia pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja. Kwa kushirikianana China pamoja na nchi nyingine washirika, Je, ni Burundi imeshiriki mafanikio gani ya kimaendeleo yaliyopatikana nchini Burundi na kikanda?

    Balozi: Burundi kuna methali inayosema 'Usiyetaka kinachotoka nyumbani kwako, usitegemee kinachoingia' sasa hapa Burundi imenufaika sana sababu hivi ni nchi ambayo iko katika ukanda wa Afrika Mashariki na hapo, kwanza viongozi wanasaidiana kwa kuongozana, wananchi wenyewe pia kupeana biashara, mfano Burundi ni nchi ambayo haifiki kwenye bahari yotote, hivyo bila kupeana biashara na nchi zingine za Afrika Mashariki inaweza kupata matatizo, hapo sasa huu mfumo wa kuwa pamoja wa kupeana biashara ni mfumo mzuri na Burundi kama nchi moja ya Afrika Mashariki inapata manufaa sana kutokana na muungano huu. Kutokana na hii sera ambayo inahusisha kupeana na mawasiliano, na hata kujenga barabara, bidhaa na huduma zinaweza kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine, na hivi sasa mtu akitaka kutoka Burundi kwenda Uganda ni rahisi, akitaka kutoka Burundi kwenda Kenya ni rahisi vile vile.

    Mwanahabari: Mwaka huu ni mwaka wa 55 tangu China na Burundi zianzishe uhusiano wa kibalozi. China imeunga mkono kwa kiasi kikubwa maendeleo ya teknolojia ya habari na maswailiano. Wakati wa kombe la dunia, Big Screen iliyopo katikati ya jiji la Bujumbura, imeanza kutumika rasmi, na wakazi walitazama mashindano ya michezo kwa kutumia screen hii. Pia China inachangia digital tv kwa vijiji 300 nchini burundi. Nini maoni ya wananchi wa Burundi kuhusu muktadha huu ushirikiano wa Burundi na China?

    Balozi: Warundi wanafurahi sana, hili ni jambo linalowafurahisha sana, sababu naona uhusiano wa Burundi na China, ni wa tangu zamani na unaimarishwa mwaka hadi mwaka, na hivi sasa uhusiano huu unalenga maeneo yote yanayohusu maendeleo ya nchi. Na kuhusu suala la mawasiliano, unajua watu hawawezi kuishi vizuri bila kupeana habari, bila kuwasiliana na wengine na kutaka kujua kinachoendelea hapa au pale kote duniani, sasa hili ni eneo kabisa linalostahili kuendelezwa, kukuzwa sana naona hilo naona sasa China inatoa mchango mkubwa sana, na ndio maana unaona kama warundi wanafurahia sana uhusiano huu, kama ulivyo mfano mzuri wa mchezo wa mpira wa miguu wakati wa kombe la dunia, warundi walinufaika hasa na maendeleo hayo yanayokuzwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako