• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe maalumu wa rais wa China akutana na rais wa Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2018-08-27 09:04:21

    Mjumbe maalumu wa rais wa China Bw. Su Hui jana mjini Harare alikutana na rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe.

    Bw. Su ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China amekabidhi salamu za rais Xi Jinping wa China za kumpongeza rais Mnangagwa kwa kuchaguliwa kuiongoza Zimbabwe. Amesema mafanikio ya uchaguzi wa rais wa Zimbabwe yameonesha matarajio na chaguo la wananchi, na China inakaribisha rais Mnangagwa kushiriki kwenye mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC na kuhimiza uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote, kati ya China na Afrika na kati ya China na Zimbabwe kufikia kwenye ngazi mpya.

    Rais Mnangagwa amesema Zimbabwe na China ni marafiki wa siku zote na anatarajia kuja China kuhudhuria mkutano wa FOCAC na kukutana na rais Xi Jinping na kufanya naye mazungumzo kuhusu mipango mipya ya ushirikiano kati ya Afrika na China na kati ya Zimbabwe na China. Na kuutakia mkutano huo mafanikio.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako