• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la ndege la Ethiopia kununua asilimia 49 kwenye shirika la ndege la Chad

    (GMT+08:00) 2018-08-27 20:02:37

    Shrika la ndege la Ethiopia limetangza kwamba limekamilisha makubaliano ya kununua asilimia 49 ya hisa kwenye shirika la ndege la Chad.

    Katika makubaliano hayo Chad itasalia na asilimia 51 ya mgao wa hisa.

    Shirika hilo la ndege la Chad linatarajiwa kuanza kutoa huduma Oktoba 1.

    Mkurungezi wa shirika la ndege la Ethiopia bwana Tewolde Gebremariam, amesema makubaliano hayo ni sehemu ya mpango wa shirika lake la kuongeza vituo zaidi vya kimkakati ifikapo mwaka 2025.

    Tayari shirika hilo limenunua mgao kama huo kwa mashirika kadhaa ya ndege barani Afrika kama vile Malawi na Guinea ambako ina mgao wa asilimia 45.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako