• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Benki ya Dfcu Uganda yatangaza kupungua kwa faida

    (GMT+08:00) 2018-08-27 20:04:20

    Benki ya Dfcu nchini Uganda imetangaza kupungua kwa faida yake kwa shilingi bilioni 72 katika kipindi cha mwaka wa fedha kilichokamilika Juni 30.

    Hata hivyo benki hiyo imesema oparesheni zake zimerejea hali ya kawaida baada ya kipindi cha kuunganisha mali ilizonunua kutoka benki ya Crane.

    Kwenye taarida Dfcu imesema kuwa imepata faida ya shilingi bilioni 41.ikilinganishwa na bilioni 114 za kipindi sawa na hicho mwaka 2017.

    Mkurungezi mkuu wa benki hiyo William Sekabembe, amesema kwenye kipindi kilichosalia cha mwka 2018 watazingatia zaidi kuwekeza kwenye teknolojia ili kuvutia wateja zaidi.

    Dfcu kwa sasa ndio benki ya pili kwa ukubwa nchini Uganda baada ya ile ya Stanbic.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako