• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa Usafiri wa Anga wa Nigeria atarajia kuwa Mkutano wa FOCAC utanufaisha China, Nigeria na Afrika kwa ujumla

    (GMT+08:00) 2018-08-28 09:16:21

    Waziri wa usafiri wa anga wa Nigeria Bw. Hadi Sirika amesema anatarajia kuwa Mkutano ujao wa FOCAC utanufaisha China, Nigeria na Afrika kwa ujumla, na pia ameikaribisha China kuongeza uwekezaji nchini Nigeria na katika nchi nyingine za Afrika.

    Bw. Sirika amesema Nigeria inatilia maanani Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utakaofanyika mwezi ujao mjini Beijing, na kutumai kuwa mkutano huo utaweza kuleta fursa zaidi za maendeleo kwa ajili ya ushirikiano kati ya China na Nigeria. Anasema,

    "Nchini Nigeria tuna miradi ya reli na viwanja vya ndege iliyojengwa na China na mradi mpya wa barabara uliosainiwa hivi karibuni. Natumaini kuwa Mkutano wa FOCAC utazinufaisha China, Nigeria na Afrika kwa ujumla katika nyanja mbalimbali zikiwemo jamii, utamaduni na siasa."

    Aidha Bw. Sirika amesema Afrika ina rasilimali nyingi na China ina uwezo mkubwa wa uchumi na teknolojia, na Nigeria inaikaribisha China kuwekeza zaidi nchini humo na katika nchi nyingine za Afrika. Anasema,

    "Afrika ni bara kubwa lenye watu bilioni moja, na pia lina tamaduni mbalimbali, na maliasili zake nyingi zinasubiri kuendelezwa. China ina uwezo kubwa wa teknolojia na nguvu kazi nyingi, sifa ambazo zimeiwezesha China kupata mafanikio makubwa ndani ya miongo kadhaa. Naamini kuwa katika muda mfupi ujao tunaweza kufikia mafanikio kama iliyopata China, ambayo pia ni lengo la Ajenda ya 2063 ya Afrika. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako