• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatangaza hatua mpya kuhusu kufanya ushirikiano wenye ufanisi na nchi za Afrika

    (GMT+08:00) 2018-08-28 17:05:20

    Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika wa mwaka 2018 utafanyika mwezi Septemba. Ofisa wa Wizara ya biashara ya China ametangaza kuwa wakati wa mkutano huo China itatangaza hatua mpya za ushirikiano wenye ufanisi na nchi za Afrika ambazo zinalingana na mikakati ya maendeleo ya nchi mbalimbali za Afrika, ili kuongeza uwezo wa nchi hizo wa kupata ukuaji wa uchumi.

    Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Qian Keming ameeleza kuwa, mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika wa mwaka 2018 utatekeleza hatua mpya za ushirikiano wenye ufanisi na nchi za Afrika, anasema:

    "Hapo awali China iliweka mipango na kufanya ushirikiano na nchi za Afrika, lakini kutokana na hatua hizo mpya, China itatuma kundi kubwa la kufanya utafiti katika balozi za China katika nchi mbalimbali za Afrika ili kufanya majadiliano na kupata ushauri kutoka kwao. Mbali na hayo tumetuma ujumbe kupata ushauri kutoka kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika."

    Kutokana na takwimu zisizokamilika, kampuni za China zimeanzisha maeneo 25 ya kiuchumi na kibiashara barani Afrika ambayo yameshirikisha kampuni zaidi ya 400, na kuwaajiri wafanyakazi elfu 41 wenye uraia wa nchi za kigeni, hatua ambayo imeisaidia Afrika kuongeza nafasi za ajira, na kuhimiza mchakato wa maendeleo ya viwanda barani Afrika.

    Takwimu zimeonesha kuwa China imekuwa mwenzi mkubwa wa kwanza wa biashara barani Afrika katika miaka 9 iliyopita. Bw. Qian Keming ameeleza kuwa, China imechukua hatua nyingi kupanua uagizaji wa bidhaa kutoka Afrika, kati ya nchi 33 zilizoko nyuma kiuchumi duniani ambazo zimeanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China, asilimia 97 ya nchi zimesamehewa ushuru wa forodha. Bw. Qian Keming anasema:

    "Katika maonesho ya kimataifa ya uagizaji wa bidhaa ya China, tumetoa nafasi kwa nchi zilizoko nyuma zaidi kiuchumi duniani barani Afrika bila malipo, ili kuzisaidia zitangaze bidhaa zao nchini China. Wakati huo huo tunazisaidia nchi za Afrika kuharakisha mchakato wa utandawazi wa viwanda, ili kuzisaidia kampuni za China kuwekeza barani Afrika, na kuhimiza uwezo wa nchi za Afrika katika kuuza bidhaa nje ya nchi. Mbali na hayo pia tunatoa mafunzo ya kuwaandaa wataalamu, na kuzisaidia nchi za Afrika kuboresha miundo mbinu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako