• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa Tanzania nchini China aeleza ushirikiano kati ya nchi mbili

    (GMT+08:00) 2018-08-29 08:12:46

    "Katika makumi ya miaka iliyopita, China na Afrika zimeshirikiana na kushikamana kwa dhati. Zinadumisha hali ya kuwa jumuiya yenye hatma na maslahi ya pamoja." Hayo yamesemwa na rais Xi Jinping wa China wakati alipotembelea Afrika mwezi Juni, mwaka huu. Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika. FOCAC utakaofanyika hivi karibuni, unafuatiliwa sana duniani. Kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo, waandishi wa habari wa CRI wamefanya mahojiano na mabalozi wa Tanzania, Zimbabwe, Rwanda, Uganda, Burundi na Afrika Kusini nchini China, kuhusu mafanikio na maendeleo yaliyopatikana chini ya mfumo wa FOCAC, kuhimiza ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja ili kupata maslahi ya pamoja ya China na Afrika. Hivi karibuni tumemhoji balozi wa Tanzania nchini China Bw. Mbelwa Kairuki akieleza ushirikiano kati ya China na Tanzania.

    Mwanabahari: Je, unaonaje mchango wa sera ya mageuzi na ufunguzi mlango ya China kwa maendeleo ya uchumi wake na mchango wake kwa utulivu na usawa wa maendeleo ya uchumi duniani?

    Balozi: Miaka 40 iliyopita China ili kuwa ni nchi iliyojifunga, lakini baada ya Deng Xiaoping kuanza kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, na kukaribisha utaalamu, mitaji, na kufanya biashara kutoka nje, hata kuwawezesha wachina kwenda nje kujifunza na kushirikiana na wengine. Matokeo yake ndio mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa kipindi kifupi kwenye nyanja ya uchumi, sayansi ya teknolojia, na hata kwenye maswala ya kimataifa. Kwa sasa China ni moja ya nchi zinazotoa mchango mkubwa kwenye ulinzi wa amani duniani, hii ni sehemu. Kwenye biashara China imekuwa mmoja wa wanachama muhimu wa shirika la biashara dunia, na ina mchango muhimu sana. Takwimu za mwaka 2016 zinaonyesha kuwa China imeanza bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani trilioni 1.8, na imenunua baadhi za trilioni 1.7 kutoka nje. Nchi nyingi sana tajiri na maskini zimenufaika. Lakini kwenye kilimo peke yake, mwaka 2016 China iliagiza bidhaa za kilimo zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 110, kati ya hizo Afrika imenunua bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 2.7.

    Mwanahabari: Tanzania na China zinaonekana kuwa na uhusiano mzuri kwa muda mrefu, na sasa hali ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili ikoje?

    Balozi: Tanzania tumekuwa na msimamo wa kimsingi, kuiunga mkono China kwenye maslahi yake ya kimsingi. Tunasimamia, tunaamini na tunaunga mkono Sera ya China moja. China kwenye ni nchi moja haya maeneo ya Hong Kong, Macau, Taiwan na Tibet, huo msimamo wetu uko palepale haubadiliki. Lakini vile vile kuna maswala yao ya msingi, yaani maswala ya maslahi, kama mgogoro wa bahari ya China Kusini, sisi msimamo wetu umekuwa ni kuiunga mkono China, kwamba matatizo haya yamalizwe kwa njia ya mazungumzo baina ya wahusika, na nchi nyingine zenye ajenda yake zisiingilie kinyume na hali halisi. Kwenye chaguzi za kimataifa tumekuwa tunaunga mkono, China ikiona Tanzania inagombea moja kwa moja inaiunga mkono Tanzania, na Tanzania ikiona China inagombea moja kwa moja inaiunga mkono China. Kwenye mambo ya kimataifa kama "ukanda mmoja, njia moja", na maonyesho ya uagizaji bidhaa ya Shanghai Tanzania inaalikwa tangu mwanzo. Na hivi karibuni kumekuwa na mkutano mkubwa kati ya chama cha kikomunisti ya China na vyama tawala vya nchi za Afrika umefanyika kwa mara ya kwanza nje ya China, umefanyika Tanzania.

    Mwanahabari: Kutokana na Baraza la Ushirikiano la China na Afrika, ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika umekuwa umeongezeka kwa kasi katika miaka iliyopita. Je! Kuna mifano yoyote inayoonyesha faida za ushirikiano huu unafikia watu wa kawaida katika nchi yako?

    Balozi: Kuna miradi mingi ya kuwanufaisha watanzania moja kwa moja iliyotokana na baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika. Mifano ni pamoja na Taasisi ya matibabu ya moja ya Jakaya Kitwete iliyopo Dar es salaam, kabla ya kujengwa kwa msaada wa China, Tanzania ilikuwa inatumia mamilioni ya dola kupeleka watu nje kwenye matibabu, na sio wote walikuwa wanapelekwa, wengine inawezekana walikuwa wanakufa bila kutibiwa, lakini sasa watanzania zaidi ya elfu moja wametibiwa nyumbani, na watalaamu wetu na wengine wanaokuja kutoka nchi nyingine, lakini wanatumia zana zilizoletwa na wachina. Kuna miradi ya maji ya Unguja na Pemba, zamani kina mama walikuwa wanaenda umbali mrefu kwenye kuchota maji kwa ndoo, lakini sasa wanapata maji kwenye umbali mfupi. Kwenye afya, hospitali yenye vifaa vya kisasa na huduma za kisasa ya Abdula Mzee , zamani watu wa Pemba walikuwa wanakwenda kutibiwa hospitali ya Mnazi mmoja ya Unguja, lakini sasa wanatibiwa Pemba. Kuna miradi mingi ya uwekezaji, katika miaka mitatu kuna miradi 196 inatoa ajira elfu 16,800 hizi ni ajira za moja kwa moja, mbali na watu wanaowategemea, na ajira zisizo moja kwa moja. Kuna watanzania elfu nne wamepata mafunzo ya muda mfupi kupitia FOCAC, hili ni jambo kubwa kwetu. Elimu waliyopata kwenye mafunzo ya muda mfupi, ni jambo la kuthamini sana. Lakini pia kila mwaka watanzania 120 wanakuja kwenye shahada za uzamili na uzamivu.

    Mwanahabari: Una maoni gani juu ya sera za China kwa Afrika? Una matarajio gani kwenye FOCAC litakalofanyika mwezi Septemba?

    Balozi: Miaka mitatu sio mingi. Mwaka 2015 kwenye mkutano wa FOCAC Rais Xi alitangaza maeneo 10 ambayo angependa China iweke mkazo kwenye ushirikiano kati yake na Afrika, mambo makubwa yamefanyika katika kipindi cha miaka mitatu, lakini hayajakamilika. Matarajio yetu ni kwamba, hatua kumi alizotangaza Rais XI kwenye mkutano uliopita wa FOCAC zitatangazwa upya,bado tunahitaji kujijengea uwezo, bado tunahitaji kuendelea na mapinduzi ya viwanda, production capacity cooperation bado tunahitaji, kilimo, afya na ulinzi na usalama, hazijakamilika bado tunahitaji uwekezaji, mitaji, matarajio yetu ni kuwa yatahimizwa Zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako