• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China imekuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 9 mfululizo

    (GMT+08:00) 2018-08-29 09:15:22

    China imeendelea kuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka tisa mfululizo. Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Qian Keming amesema biashara kati ya China na Afrika imeongezeka kwa kasi baada ya kuzinduliwa kwa mipango 10 ya ushirikiano miaka mitatu iliyopita, kwenye mkutano wa kilele wa Johannesburg wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika mwaka 2015.

    Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, biashara ya pande mbili iliongezeka kwa asilimia 16 kuliko mwaka jana kipindi kama hicho, na thamani yake imefikia dola za kimarekani bilioni 98.8.

    Katika miaka mitatu iliyopita, wastani kwa mwaka wa uwekezaji wa moja kwa moja wa China barani Afrika ulikuwa dola za kimarekani bilioni 3, huku maendeleo yakiwa yamepatikana katika ushirikiano wa sekta za uzalishaji viwandani, mambo ya fedha, utalii na usafiri wa anga.

    Miundombinu ya Afrika imeendelezwa kutokana na mipango hiyo ya ushirikiano, ambayo inatarajiwa kulipatia bara hili kilomita elfu 30 za barabara kuu, tani milioni 85 za uwezo wa bandari kwa mwaka, tani milioni 9 za uwezo wa kusafisha maji kwa siku na megawati elfu 20 za uwezo wa kuzalisha umeme na kutengeneza nafasi za ajira zipatazo laki 9.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako