• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yapanga kuzindua maeneo manne ya viwanda yaliyojengwa na China

    (GMT+08:00) 2018-08-29 09:43:55

    Ethiopia inapanga kuzindua maeneo manne ya viwanda yanayojengwa na China kabla ya mwishoni mwa mwaka huu. Kamishna wa tume ya uwekezaji wa Ethiopia Bw. Belachew Mekuria amesema, maeneo hayo manne ni pamoja na Jimma na Arerti yanayojengwa na Kampuni ya CCCC ya China, na Adama na Dire Dawa yanayojengwa na Kampuni ya CCECC ya China.

    Bw. Mekuria pia amesema, licha ya ukosefu wa fedha za kigeni, huduma za jamii na kukosekana kwa utulivu katika baadhi ya maeneo ya Ethiopia tangu mwaka 2016, miradi ya ujenzi wa maeneo ya viwanda inayotekelezwa na makampuni ya China imeendelea kama ilivyopangwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako