• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biashara katika nchi za EAC yaongezeka kwa $4bn

    (GMT+08:00) 2018-08-29 20:02:45

    Biashara miongoni mwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki imeongezeka kwa $4b tangu kuanzishwa kwa umoja wa forodha tarehe 2 Januari,2005.

    Ukuaji huo unaashiria umuhimu wa ushirikiano wa kikanda kwa nchi wanachama ambazo hasa hufuata ushirikiano wa kibiashara na soko.

    Mkuu wa Forodha EAC ,Bw Kenneth Bagamuhunda, wakati wa mkutano wa 22 wa kamati ya masuala ya kifedha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,alisema japokuwa ushirikiano utachukua muda kuafikiwa,tayari matokeo chanya yashaanza kuonekana.

    Alisema tangu Januari 2005,ushirikiano wa kibiashara EAC umesababisha kuongezeka kwa kiwango cha biashara.

    Aliongeza kuwa mwaka 2005 biashara kati ya nchi za EAC ilikuwa $1.5b lakini imeongezeka hadi $5.5b mwka 2017.

    Kulingana na Bagamuhunda,miundombinu katika kanda imeimarika,jambo ambalo limesaidia ukuaji wa biashara katika kanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako