• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sierra Leone yasema China ni mwezi wake muhimu wa biashara

    (GMT+08:00) 2018-08-30 08:46:23

    Msemaji wa rais wa Sierra Leone Bw. Abdulai Baraytay amesema tangu China na Sierra Leone zilipoanzisha uhusiano wa kibalozi, nchi hizo mbili zimedumisha mawasiliano ya kirafiki.Sierra Leone inashikilia kithabiti sera ya China moja, na inaichukulia China kuwa ni mwenzi wake muhimu wa biashara, na itaendelea kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa kati yake na China na kuendeleza ushirikiano wa kunufaishana kati ya pande mbili.

    Bw. Baraytay amesema hayo akihojiwa na mwanahabari wetu katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa. Anasema,  

    " miundombinu mingi ya Sierra Leone imejengwa na makampuni ya China, kama vile uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mamamah mjini Freetown. Ukifika Sierra Leone, utaona kampuni kubwa zaidi ya ujenzi nchini humo ni Kampuni ya Saba ya Ujenzi wa reli ya China, ambayo bila shaka ni alama ya ushirikiano wa kiwango cha juu wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Sierra Leone."

    Bw. Baraytay amesema tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Sierra Leone miaka 47 iliyopita, China imejenga miundombinu mingi nchini Sierra Leone, zikiwemo barabara, madaraja, viwanja vya michezo, vituo vya kueneza teknolojia ya kilimo, na vituo vya umeme wa maji. Anaamini kuwa chini ya mfumo wa FOCAC, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili utazidi kuimarika siku hadi siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako