• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbegu za maisha bora zaota mizizi Afrika

    (GMT+08:00) 2018-08-30 08:56:29

    Mwezi Desemba mwaka 2015, Rais Xi Jinping wa China alitoa taarifa katika mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika Johannesburg, kuwa China itazidisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote na nchi za Afrika. Rais Xi alisema Mipango kumi ya Ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye sekta ya viwanda, kilimo cha kisasa, miundo mbinu, uchumi, maendeleo yasiyosababisha uchafuzi, uwekezaji na biashara, kupunguza umaskini, afya, utamaduni, amani na usalama imefungua mlango mpya wa uhusiano kati ya China na Afrika.

    Wakati mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika unakaribia kufanyika mjini Beijing, tunafuatilia Mipango kumi ya Ushirikiano kati ya China na Afrika, na kuona jinsi uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Afrika unavyozidi kukua. Tunaanza kuhusu Mbegu za maisha bora zaota mizizi Afrika.

    Upepo wa mwezi wa saba unavuma katika mashamba ya Morogoro, na mimea inatoa sauti. Sauti hiyo ni sauti ya mavuno ya wanakijiji wa Mtego wa Simba. Adam mwenye umri wa 35, yuko juu ya kando ya shamba, akipiga mahesabu kuhusu mapato ya mwaka huu.

    "Sasa ninaweza kupata magunia 11 au 12 ya mboga kwenye kila eka ya shamba. Kama mwaka ni mzuri ninaweza kupata magunia 16, mboga ya shamba moja dogo sana inaweza kuzalisha mboga nyingi."

    Gunia moja la Magunia moja ya maboga kwa kawaida ina uzito wa kilo 100. kabla ya miaka mitatu, Adam hakuwezi kupata mavuno kama hayo. Wakati ule hakuwa na matumai yoyote kwa arthi hiyo.

    "Zamani niliweza kupata magunia manne ya mboga, kwa bahati nzuri niliweza kupata magunia 7 tu. Kwa mfano nilipata magunia manne, halafu niliuza gunia moja na kuhifadhi magunia matatu kwa ajili ya chakula. Lakini kama mtu yeyote nyumbani akiumwa au ajali fulani ikitokea, nitapaswa kuuza magunia mengine. Halafu hatuyakuwa na chakula, tutapaswa kununua chakula sokoni. Gunia moja la mboga linauzwa shilingi laki 1.2 kwa kawaida, hii ni bei kubwa sana kwangu."

    Shilingi laki 1.2 za Tanzania ni sawa RMB yuan 350 tu. Lakini kwa wanakijiji wa Tanzania wanaopata mapato ya takriban Yuan 1000 tu kwa mwaka, yuan 350 ni pesa nyingi. Kwa njia gani wanaweza kupata mapato zaidi? Ili kuitikia mwito wa serikali ya Tanzania kuzidisha ushirikiano wa kilimo kati ya China na Tanzania, mwaka 2014 wataalamu wa kilimo wa China walifika katika kijiji cha Simba. Kabla ya hayo, walifanya ushirikiano na Kituo cha Kupunguza Maskini cha Kimataifa cha China, na kujaribu kuanzisha mradi ya kupunguza umaskini kwenye kijiji cha Peapea. Kwa kutumia njia ya kilimo za China, idadi ya uzalishaji wa mboga wa kijiji hicho kwa kila eka, umeongezeka kutoka kilo 66 hadi kilo 200. Mara hiyo, Chuo Kikuu cha Kilimo cha China, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine cha Tanzania na serikali ya mkoa wa Morogoro vimeunda tena timu ya utafiti. Timu hiyo ilichagua kijiji cha Simba kuwa kijiji cha mfano cha kueneza teknolojia ya kilimo cha China. Moja ya viongozi wa timu hiyo alikuwa mwalimu Li Xiaoyun wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China, ambaye amefanya utafiti nchini Tanzania tangu mwaka 2008, na yeye anaona kuwa ili kupunguza umaskini, ni lazima Tanzania izidishe uwezo wa uzalishaji wa kilimo.

    "Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania. Tanzania inapaswa kuendeleza kilimo chake ili kupunguza umaskini. Sasa Tanzania ina tatizo la nafasi za ajira. Nguvu kazi yake haiwezi kuhama kutoka kwenye sekta ya kilimo. Kwa hivyo Tanzania inapaswa kuzidisha ufanisi wa uzalishaji wa kilimo kwa ajili ya kuzidisha mapato ya kilimo. Hili ni lengo muhimu sana kwa Wataznania."

    Li Xiaoyun anaona Tanzania sasa inaendeleza kilimo chake kwa njia ya kupanua maeneo ya mashamba, lakini siyo kwa njia ya kuzidisha uwezo wa uzalishaji. Ukosefu wa fedha pia unazuia maendeleo ya kilimo. Kwenye hali hiyo, anatoa njia inayofaa hali ya Tanzania.

    "Lengo letu kubwa ni kuzidisha uwezo wa uzalishaji wa ardhi na wa kazi. Mahali hilo linakosa mitaji sana, hakuna uwezo wa kueneza uwekezaji ukubwa au matumizi ya mashine. Kwa hiyo tunafikiri tunaweza kuzidisha uzalishaji kwa njia ya kuboresha aina za mimea, kuzidisha hesabu ya mimea kwenye kila shamba na kuchukua hatua zinazofaa."

    Wataalamu wa China wamekuja. Wanakijiji wa kijiji cha Simba wote hawawezi kusubiri kuwa mkulima wa mfano. Adam alikuwa mmoja wa wanakijiji hao. Mwaka 2015 alipata ugonjwa, na matibabu yake yalichukua pesa nyingi. Mwaka 2016 alikuwa mkulima wa mfano, na kutumai teknolojia ya China inaweza kubadili maisha yake, na sasa matumaini yake yanatimia.

    "Ninaamini teknolojia ya kichina na wataalamu wa China. Zamani tulilima kwa njia ya jadi. Hatukujua namna ya kupima, na kama mbegu zilifa kutumika. Sasa tunafahamu namna ya kupima nafasi, na kununua mbegu nzuri dukani. Baada ya kujua namna ya kuongeza idadi ya mimea kwenye shamba hali imebadilika, zamani tulipanda kilo 4 tu za mbegu kwa eka, sasa tunaweza kupanda kilo 8 za mbegu. Yaani utoaji kwa eka 1 sasa ni sawasawa na utoaji wa eka 2 zamani. Sasa tuliweza kuhifadhi magunia 3 ya mboga kwa ajili ya chakula na kuuza magunia 10 au 13. Kila kilo ninaweza kupata shilingi 500 au 540, baadhi ya wakati ninapata shilingi 700 au 800, ni mapato makubwa sana. Pesa hizo zinatosha kabisa kwa matumizi ya familia yangu.

    Kulikuwa na wakulima wengi kama Adam walioona mabadiliko yanayoletwa na teknolojia ya kilimo ya China. Lakini pia wakulima wengi sana walikuwa na wasiwasi baada ya kuchukua hatua hayo, kuwa watalazimika kununua mbegu nyingi na kuajira wafanyakazi kuwasaidia yaani watawekeza fedha mingi zaidi, halafu kama wataweza kupata mapato mengi kwa kweli. Adam aliwaambia watu kuwa kilo moja ya mbegu itagharimu shilingi 800, na kila eka ardhi watahitaji kilo nane za mbegu, kwa hiyo watawekeza shilingi 3200 kwenye kila eka. Lakini kama watapata mboga kilo 100 ni kitu kingine, watapata mapato ya shilingi 50000. Kwa hiyo kwa kweli watapata mapato mengi zaidi.

    "Usiogope kuwekeza fedha nyingi, bila shaka utapata zaidi kama ukiwekeza mingi."

    Wanakijiji walianza kuamini teknolojia ya kichina, halafu, wataalam wa China waliletea kijijini mwelekeo wa teknolojia.

    "Mwanzoni kullikuwa na wakulima kumi tu wa mfano, halafu kila mmoja aliwafunduisha wakulima kumi, yaani kulikuwa na zaidi ya wakulima 100 wa mfano. Hata wao ambao hawakushirika wakulima wa onyesho walikwenda kujifunza ujuzi. Baada muda mfupi ujuzi wa kichina ulienezwa sana."

    Kutumia teknolojia mpya ya kilimo ni hatua ya kwanza tu ya kupunguza umaskini. Baada ya wataalamu wa China kuondoka, la muhimu ni kwa namna gani wakulima watajifunza teknolojia, kwa namna gani kijiji hicho kitajiendeleza.

    Mwezi Julai mwaka 2018, Wizara ya Biashara ya China na Wizara ya Kilimo ya Tanzania zilifanya ushirikiano kuanzisha darasa ya ufundishaji ya kueneza teknolojia ya kilimo cha kisasa na kubadilisha mfumo wa kilimo. Wataalamu wa China walifika Morogoro kufundisha wataalamu wa kilimo wa Morogoro kwa mwezi nusu, wataalamu hao walifanya utafiti shambani, walijifunza ujuzi darasani na kuzungumza na wataalamu wa China kuhusu njia ya kuendeleza kilimo kutokana na hali halisi. Li Xiaoyun amesema darasa la ufundishaji kama huo una maana kubwa.

    "Sasa tunafanya ufundishaji kwenye mashamba ya Tanzania, kwa hiyo tunaweza kuonyesha wakulima tunazidisha uzalishajii kwa njia gani, halafu tunaweza kufundisha wataalamu kutoka mkoa wa Morogoro pia. Lengo yetu ni kuanzisha timu inayoweza kueneza kufundisha ujuzi mpya."

    Wakulima wengi wanafurahi kuweza kujifunza ujuzi e shambani.

    "Zamani hatukuweza kujifunza ujuzi na teknolojia mpya kabisa, hatukufahamu mambo mengi. Darasa hilo limebadilisha dhana yetu, na kutupa fursa ya kufanya mawasiliano na wataalamu wengine."

    "Darasa kama hilo inaweza kutufunza ujuzi wingi. Tumefahamu uzoefu wa kulima wa China na teknolojia inayoweza kuzidisha utoaji pia. Hasa tumefahamu njia ya kufanya mbolea."

    Mpaka sasa, China imetoa miradi ya kilimo zaidi ya mia moja kwa nchi zaidi ya 80, na imetuma wataalamu wa kilimo zaidi ya 5000. Wameleta mabadiliko makubwa kwa watu wa nchi hizo. Uzalishaji wa kilimo umeongezeka, na mapato ya wanakijiji wa kijiji wa Simba pia.yameongezeka Familia ya Adam itahamia kwenye nyumba kubwa mpya. Nyumba hiyo ina umeme.

    "Baada wataalamu wa China kufika, mapato yetu yameongezeka sana, sasa yanafikia shilingi laki 8 hadi milioni moja (sawa na RMB yuan 2357-2946). Kama unavyoona, zamani tuliishi kwenye nyumba ya majani, hakukuwa na umeme. Lakini sasa tutahamia kwenye nyumba mpya, na tutaweza kutumia umeme kijijini kwa wakati mfupi sana."

    Kutokana na msaada wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China, mradi "wakulima 1000 na mashamba ya mahindi ya eka 10000" umeanzishwa Tanzania mwaka huu. Mradi huu ulipanga kusaidia wakulima 1000 kutoka wilaya 10 za mkoa Morogoro kuzidisha utoaji kwenye mashamba ya eka 10000. Li Xiaoyun ana matarajio sana na mradi huu.

    "Ninatumai vijiji 10 tunavyoanzisha mradi wetu, vinaweza kupata mavuno ya mara ya mbili ya zamani kwenye miaka 3 ijayo. Wakulima hawa 1000 wanaweza kuhimiza wakulima 10000. Tunatarajia mashamba hayo eka elfu 10 ya mfano yataweza kuhimiza mabadiliko kwenye eka laki 1."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako