• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Ghana zashirikiana kwa mara ya kwanza kutengeneza filamu kuhusu ugonjwa wa Ebola

    (GMT+08:00) 2018-08-30 18:59:25

    Wanafilamu kutoka China na Ghana wameshiriki katika hafla ya kusaini makubaliano kuhusu ushirikiano wa filamu iliyofanyika Agosti 29, na kutangaza kwa pamoja kuwa watashirikiana kutengeneza filamu iitwayo"Ebola".

    Huu ni ushirikiano wa kwanza katika sekta filamu kati ya nchi hizo mbili, pia ni filamu ya kwanza itakayotengenezwa kwa pamoja kati ya China na Afrika.

    Maandalizi ya uandishi wa filamu hiyo inayosimulia hadithi nyingi za kugusa kuhusu timu ya matibabu ya China katika nchi za Afrika Magharibi wakati mlipuko wa Ebola ulipotokea kwenye eneo hilo mwaka 2014 bado yanaendelea. Timu itakayotengeneza filamu hiyo inapanga kwenda Afrika mwaka 2019, na filamu hiyo inatarajiwa kukamilika mwaka 2020 na kuonyeshwa wakati wa maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Balozi wa Ghana nchini China Bw. Edward Boateng anatumai pande hizo mbili zitakuwa na fursa nyingi zaidi za kusimulia hadithi moja kwa pamoja kupitia filamu katika siku za baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako