• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda-Bodi ya Kilimo Rwanda kugawa zaidi ya tani 2,000 za mbegu za mahindi

    (GMT+08:00) 2018-08-30 20:10:49

    Bodi ya Kilimo ya Rwanda kwa mara ya kwanza kabisa itasambaza na kuwagawia wakulima takriban tani 2,000 za mbegu za mahindi zilizozalishwa nchini humo kwa ajili ya msimu wa upanzi A unaoanza mwezi Desemba.

    Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kilimo ya Rwanda ,Dkt Patrick Karangwa, alisema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa uzalishaji mbegu ili kupunguza uagizaji ikiwa na malengo ya kupata asilimia 60 ya mbegu za mahindi zinazozalishwa nchini kufikia mwaka 2021.

    Mkakati huo umeweka msisitizo katika mimea nane ikiwamo mahindi,ngano,viazi,soya na maharage.

    Takwimu zinaonyesha kuwaserikali hutumia takriban Rwf3.4bn kuagiza mbeguy za nafaka kila msimu.

    Hata hivyo uagizaji huo unaweza kupunguzwa kutokana na tani za mbegu za mahindi ambazo zimezalishwa nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako