• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Waziri mstaafu Pinda atoa wito kwa serikali kusaidia wafugaji kuku

    (GMT+08:00) 2018-08-30 20:12:36

    Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Mizengo Pinda ,amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili wafugaji wa kuku bora mkoani Dodoma ni upungufu wa vifaranga.

    Pinda alitoa kauli hiyo mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulenga,katika shughuli ya utoaji vifaranga 3,000 kwa chama cha wafugaji kuku bora Dodoma (Chawakuboda).

    Alisema kwa kiasi kikubwa ufugaji huo unakabiliwa na changamoto ambazo ni upungufu mkubwa wa vifaranga na uhaba wa upatikanaji wa chakula bora kwa ajili ya vifaranga.

    Alimwomba Ulega kukitumia chama hicho cha ushirika wa vikundi hivyo katika kusaidia kutimiza malengo ya serikali na waandalie namna ya kuanzisha kiwanda kikubwa cha kuzalishia kuku.

    Kwa upande wake Ulega alikiri kuwapo kwa changamoto ya upatikanaji wa vifaranga nchini Tanzania.

    Alisema wizara itahakikisha inatoa chanjo ya dozi 100 kwa wanachama 40 wa chama hicho,ili kudhibiti vifo vya kuku vitokanavyo na maradhi ya mdondo na kideri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako