• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujenzi wa reli tatu barani Afrika washuhudia mchakato wa China na Afrika katika kukabiliana kwa pamoja matatizo na kutafuta maendeleo ya pamoja

    (GMT+08:00) 2018-08-31 18:18:49

    China inatajwa kama nchi inayofanya ujenzi kwa wingi zaidi wa miundo mbinu, na miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundo mbinu ikiwemo reli ya TAZARA iliyojengwa katika miaka ya 1960 pia imeshuhudia urafiki kati ya China na Afrika katika miaka mingi iliyopita. Wakati China ilipotoa msaada katika ujenzi wa reli ya TAZARA katika miaka 40 iliyopita, haikuwa na vifaa na teknolojia za kisasa, ilichokuwa nacho ni moyo wa dhati kwa watu wa Afrika. Ujenzi wa reli hiyo ulikamilika mwezi Julai mwaka 1976 baada ya wafanyakazi 60 kujitoa muhanga, na umekuwa ukichangia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi pamoja na mapambano ya ukombozi wa taifa katika sehemu ya katikati na kusini mwa Afrika, na kuwa alama muhimu ya China katika kuziunga mkono kazi ya kujipatia ukombozi na uhuru ya nchi za Afrika.

    Baada ya mchakato wa miaka 40 wa mageuzi na ufunguaji mlango , China imekua nchi ya pili la uchumi duniani, inaendelea kushikilia kanuni ya kuhimiza ushirikiano wa kirafiki na kupata maendeleo ya pamoja na nchi za Afrika, na ilitangaza mipango mbalimbali ya ushirikiano na nchi za Afrika tangu kuanzishwa kwa baraza la ushirikiano kati ya pande hizo mbili mwaka 2000, na miradi mbalimbali ya miundo mbinu imetekelezwa ikiwemo reli inayounganisha Addis Ababa, Ethiopia, na Djibouti, ambayo inasifiwa kama ni "Reli ya TAZARA ya zama mpya", Reli ya SGR inayounganisha miji ya Mombasa na Nairobi nchini Kenya, ambayo inatazamiwa kuunganishwa na reli nchini Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini, na kuunda mtandao wa reli katika Afrika Mashariki.

    Kwa nini ushirikiano kati ya China na Afrika unaweza kupata mafanikio hayo? Siri yake ni udhati na kanuni ya kunufaisha pande zote. Katika miaka mitano iliyopita, Rais Xi aliichukua Afrika kuwa kituo cha kwanza cha ziara yake ya kwanza kwa mwaka; China imekuwa mwenzi mkubwa wa kwanza wa biashara kwa Afrika katika miaka 9 iliyopita na China imesamehe ushuru wa forodha kwa bidhaa kutoka nchi 33 zilizoko nyuma zaidi kiuchumi duniani, hatua ambayo imeonesha kuwa China si kama tu inakabiliana na changamoto mbalimbali kwa pamoja na Afrika, bali pia inatafuta maendeleo kwa pamoja.

    Hivi sasa hali ya kimataifa inabadilika badilika, na kuonesha utatanishi mkubwa, huku utaratibu wa upande mmoja na umwamba wa kibiashara ukifufuka. Kuongeza ufanisi na kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja iliyo na uhusiano wa karibu zaidi kati ya China na Afrika kuna umuhimu mkubwa zaidi. Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utakaofanyika tarehe 3 na 4 mwezi ujao hapa Beijing unatarajiwa kusukuma mbele ujenzi wa "Ukanda mmoja, Njia moja" na Ajenda ya mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika, kuoanishwa na ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa na mikakati ya maendeleo ya nchi mbalimbali barani Afrika, ili kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika, na kuwanufaisha kwa pamoja watu bilioni 2.4 wa pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako