• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa televisheni ya digitali wanufaisha wanavijiji wa Kenya

    (GMT+08:00) 2018-09-01 16:43:24

    Mwezi Desemba mwaka 2015, kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika Johannesburg, Afrika Kusini, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuinua kiwango cha uhusiano kati ya China na Afrika kuwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote, na kutoa mipango 10 mikubwa ya ushirikiano katika sekta za viwanda, kilimo, miundombinu, fedha, maendeleo yasiyoleta uchafuzi wa mazingira, kurahisisha biashara na uwekezaji, kuondoa umaskini na kuwanufaisha watu, afya, utamaduni, amani na usalama.

    Wakati mkutano wa kilele wa FOCAC utakapofanyika mjini Beijing baadaye mwezi ujao, tunakuletea ripoti mfululizo kuhusu mipango hiyo na maendeleo mapya ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Afrika. Katika kipindi cha leo, utasikia ripoti ya tisa kuhusu jinsi mradi wa televisheni ya digitali wanavyowanufaisha wanavijiji wa Kenya.

    Kijiji cha Likii kiko sehemu ya katikati ya Kenya, kaskazini magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kenya. Kijiji hiki kina mazingira mazuri ya kiasili, lakini kiko mbali na miji mikubwa, na miundo mbinu katika kijiji hicho ni dhaifu. Katika miaka mingi iliyopita, wanakijiji wa kijiji hicho hawakuweza kuona picha nzuri kwenye televisheni. Mkuu wa kata ya Nturukuma, Nanyuki, Bw Joseph Runyenje Lopeyok amesema,

    "Huduma ya televisheni ilikuwa duni sana maana tulipata kulikuwa na familia ambazo walikuwa wakitegemea decorder moja familia kama mbili. Nafikiri timu iliyozunguka walisikia maajabu kama hayo hata mimi nilistaajabu sana kusikia watu wanatumia decorder moja,anatumia huyu leo,kesho anaichukua mwengine kutumia.Na pia kulikuwa na familia ambazo zilikuwa zinatoka kwao zinaenda kuona sinema mbalimbali kwa wenzao majirani.Ni kumaanisha kwamba kulikuwa na upungufu wa wao kuona taarifa zote zinazoendelea,na ikawa sana sana watoto wengi wanaenda kuishi kwa familia majirani kwa sababu ya hiyo na wanakuwa na vurugu kwa sababu watoto wakienda kukaa kule wazazi wanapiga kelele kwamba watoto hawawatii."

    Mwaka 2015 wakati rais Xi Jinping akitoa mipango 10 mikubwa ya shirikiano kati ya China na Afrika, alitaja mpango wa ushirikiano katika mambo ya utamaduni, na kusema China itatekeleza mradi wa kufikisha matangazo ya televisheni kwenye vijiji elfu 10 vya Afrika. Tarehe 7 Juni, mradi huo ulizinduliwa rasmi nchini Kenya na kutekelezwa na kampuni ya Startimes ya China. Mradi huo unapanga kutoa huduma ya televisheni ya satilaiti kwa vijiji 800 nchini Kenya, na kwa bahati nzuri, kijiji cha Likii kimetangulia kutekeleza mradi huo unaoweza kutatua matatizo ya huduma ya televisheni kwa wanakijiji.

    Meneja wa uhusiano wa tawi la Kenya la kampuni ya Startimes Bw Alex Mwaura amesema, kupitia mradi huo, wanakijiji wa Likii wanaweza kupata vifaa vya kupokea ishara ya satilaiti na chanel kadhaa za televisheni bila malipo, hii ni habari nzuri kwa wanakijiji wasio tajiri, akisema,

    "Kwa wale ambao watanufaika na mradi huu,hawa wanakijiji 20, hao wanapata dish, decorder, na ufungaji bure kabisa na chaneli za televisheni bure kwa mwezi wa kwanza. Lakini kwa taasisi za umma wataweza kupata dish, decorder, televisheni na mfumo wa nishati ya jua bure kabisa, na bila malipo yoyote ya mwezi. Kwa hizi kaya, baada ya mwezi wa kwanza, watakuwa na uhuru wa kulipa kila mwezi kutoka shilingi 450, ili waweze kupata hizi chaneli 35 kuendelea. Lakini kama mtu hajalipia anaweza kupata chaneli tatu za televisheni bure bila malipo, ambazo ni televisheni ya taifa KBC, na Guide Channel ambayo ina mambo ya burudani na pia CGTN ambayo ni chaneli ya kimataifa ya habari."

    Bw. Lopeyok amesema si kama tu mradi huo umewapatia Wakenya wanaoishi mbali na miji mikubwa huduma ya televisheni ya dijitali kwa urahisi, bali pia umewapatia fursa ya kujua dunia, na kupunguza pengo kati ya miji na vijiji, akisema,

    "Wamefaidika kwa kujua ni sera gani mpya za serikali ambazo zinaendelea kuja, kama kuna taarifa za habari za mambo ya sukari walikuwa na maswali mengi lakini sasa wao wanasikia kutoka kwa redio na kutazama kwa televisheni kuhusu mambo ya NYS, na pia sera nyingine za serikali kama Child Adoption ambayo ilianza juzi, tukajadiliana, nikawaeleza sheria ambayo serikali inatunga kuhusu mambo ya adoption na Guadianship."

    Kwa mashabiki wa soka wa kijiji cha Likii, hawakuwa na haja ya kusikiliza redio au kutazama televisheni katika jirani ili kujua mashindano ya soko yameendeleaje. Televisheni ya kidijitali inayoonesha idhaa nyingi imewasaidia kupata burudani nyingi zaidi. Bw. Lopeyok amesema,

    "Tukijaribu kujadiliana kuhusu vile waliona mradi huu wakanieleza kwamba wameanza kuona mpira wa World Cup ambao wao hawakuwa wakiona, na pia wameanza kuona chaneli nyingi za TV na wamekuwa wakifurahia sana wengine wamevutiwa na World Cup wakawa mashabiki wa mpira."

    Mradi huo pia umewapatia wanavijiji wa Kenya nafasi nyingi za ajira na fursa ya kupata mafunzo. Bw. Mwaura amesema kampuni ya Startimes imeandaa mafundi kwenye kila kijiji ili kutoa huduma bora kwa wanavijiji, akisema,

    "Kwa kila kijiji tunatoa mafunzo kwa vijana wawili (mvulana na msichana) ambae anaweza baada ya sisi kusimika vifaa vyetu, anaweza kuwepo kusaidia kama kuna tatizo anaweza kuja kurekbisha. Kwa hivyo kwa vijiji 800 tukiweka vijana wawili ni kumaanisha tuna uwezo wa kutengeneza nafasi za ajira zaidi ya 1,600 ambao watakuwa wakiangalia na kuhakikisha kwamba mitambo na vifaa vinafanya kazi."

    HIvi sasa ujenzi wa mradi huo umekamilika katika vijiji mbalimbali vya miji ya Nanyuki, Isiolo, Kajiado na Nairobi, na ujenzi unaendelea katika vijiji vingi zaidi na kutazamiwa kumalizika mwezi Oktoba mwaka huu. Bw. Mwaura amesema,

    Kwa hapa Kenya zaidi ya familia 16,000 zitaweza kupata hiyo huduma,na taasisi za umma 2,400 zitaweza kupata hiyo huduma.Unajua kama taasisi za umma watu ni wengi ambao wanaweza kupata hiyo huduma kwa hivyo tuna uhakika kwamba tunaweza kufikia wakenya wengi zaidi ambao hapo awali hawakuwa na uwezo wa kupata habari katika maisa yao. Natumai kwamba tutaendelea hivi hivi ili kuhakikisha kwamba wananchi wengi zaidi wana uwezo wa kupata habari,kusoma,kwa sababu televisheni siku hizi zina chaneli nyingi ambazo zina uwezo wa kufundisha wazee ,wazazi na pia watoto wetu ambao wanakua."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako